Search This Blog

Thursday, October 25, 2012

MKE WA SHABIKI WA MAN UNITED ACHOSWA NA VIPIGO VYA MUMEWE KILA MAN U INAPOFUNGWA

Mara kadhaa tumekuwa tukisikia vitu kadhaa vya kushangaza juu ya mashabiki wa soka kwa sababu tu ya mapenzi ya timu zao. Ingawa matukio hayo yanaweza yakawa yanachekesha lakini uda mwingine inakuwa ni vigumu kuelewa ni soka linaweza kuingiliana na maisha yetu binafsi kwa kiasi kikubwa namna. Hi hapa ni barua iliyoandikwa na mwanamke mmoja kutoka Kenya ambaye amekuwa akigeuzwa 'punching bag' na mume wake kila mara klabu ya Manchester United inaofungwa.

Habari,

Nimeanza kufikiria kwa kina juu ya kuomba talaka kwa mume wangu kwa sababu sifikirii kama naweza nikaendelea na ndoa ya namna hii. Nilifunga ndoa miaka 4 iliyopita na kila mara mara wakati wa mechi za ligi kuu ya England, FA Cup, Capital One Cup au UEFA Champions league ninakuwa katika kipindi kigumu sana katika maisha yangu ya ndoa.
Mume wangu ni shabiki wa kufa wa Manchester United na anaweza kufanya chochote kwa ajili ya timu yake pindi inapofungwa au kushinda.  Pindi Man U inapofungwa mwisho wake huwa naambulia vipigo, na nimekuwa nikisikia hii timu jina lake la utani ni Red Devils(Mashetani wekundu) nimeanza kujiuliza maswali kama mume wangu ni mfuasi wa dini ya shetani.

Anyway mie nimechoswa na uso wangu kuwekwa bandeji kila mara Manchester United inapofungwa kwa sababu huwa napokea vipigo vizito sana jambo ambalo linaniathiri kisaikolojia na kimwili. Sasa hivi namuogopa sana ingawa pindi Manchester United inaposhinda kama juzi usiku, mume wangu alikuwa ndio mume bora duniani.

Kiukweli hali hii inanichanganya. Nimechoka kupigwa kwasababu ya klabu ya soka.

Na hawa Manchester United kwanini wasiwe wanashinda kila siku wanapocheza?

Jane.”

2 comments:

  1. Ashukuru mumewe ni man u je Angekuwa Arsenal Angekuwa ashakufa! Makbel

    ReplyDelete
  2. Hii picha ni ya siku nyingi sana,haina uhusiano wowote na mechi ya juzi,jamani tuwe wa kweli,dunia imekuwa kijiji sio kama zamani shaffih

    ReplyDelete