Search This Blog

Saturday, May 4, 2013

LAWAMA JUU YA UTEUZI WA KIKOSI CHA TAIF STARS KWA KIM POULSEN - KIBADENI ASEMA WA KULAUMIWA NI MARSH

Baadhi ya wadau wa soka nchini wamekuwa wakimlalamikia kocha Mkuu wa Taifa Stars Kim Poulsen kwa uteuzi wa timu hiyo, ingawa kocha wa Kagera Sugar, Abdallah Kibadeni 'Mputa' ametamka kuwa wakulaumiwa ni msaidizi wake.

kocha wa Mkuu wa Ruvu Shooting, Boniface Mkwasa hivi karibuni alisema uteuzi wa kocha huyo umeegemea zaidi kwenye klabu za Simba, Yanga, Azam FC na Mtibwa Sugar.
 
Mkwasa alimtaka kocha huyo kujaribu kuwafuatilia wachezaji wa timu nyingine kwani wapo wenye sifa zote za kuichezea timu hiyo na hata kuwazidi baadhi ya waliopo kwa sasa.
 
Kibadeni alisema jijini Dar es Salaam kuwa kocha Kim hapaswi kulaumiwa kwa hilo isipokuwa msaidizi wake ambaye ni Silvester Marsh kushindwa kumshauri.
 
"Kwa upande wangu lawama hizi nafikiri zinapaswa kubebwa na msaidizi wake (Marsh) kwa kushindwa kumshauri mkubwa wake.
"Siamini kama Marsh amewahi kumshauri kitu halafu akakipinga. Kim ni kocha muelewa isipokuwa amekosa mtu sahihi wa kumshauri." alisema Kibadeni.

Katika hatua nyingine nyota wa timu hiyo Themi Felix alisema; "Nafikiri atueleze kuwa kucheza timu ya Taifa Stars ni mpaka uwe Simba, Yanga au Azam FC ndiyo unaweza kuonekana." alisema
Felix ambaye yupo kwenye kiwango kizuri cha soka.

4 comments:

  1. Kwa mimi huyo Kibadeni na mwenzie Mkwasa wote hao MAJUNGU....Mi nachoomba wawaache Kim na msaidizi wake Marsh wafanye kazi zao wao wenyewe,wameona team inafanya vizuri weshaanza kujipendekeza ooh wamechagua wachezaji wa upande mmoja tu,Hawa jamaa kwanza sidhani kama wana akili hata huo ukocha sidhani kama wanavyeti halali na kama ni halali mitihani yao waliangalizia kwa wanaojuwa hata ukiangalia kwanza team zao hazifanyi vizuri kihivyo matokeo yao ni yaki Mungu Mungu tu siyo wa vile basi Kagera wapo nafasi ya tatu wanaigombania na Simba basi ndo wakataka kujiona wapo sawa kikiwango na makocha wa Simba na Yanga na hawana uwezo wa ku comment kitu dhidi ya team yetu ya taifa mwanzo wazawa walikuwa wanapata nafasi nyingi na kubwa kwenye team yetu ya taifa matokeo yake majungu ooooh makocha wa kigeni hawana kitu oooh wanakuja hapa kuchota pesa zetu then wanaondoka zao...yaaani tukiwapa nafasi kidogo tu mtasikia taifa star kapigwa 7 na Ivory coast...kwa hiyo mi nachoomba wao mabwege wanaotaka kuaribu kikosi kwa kutaka kuwachomeka watoto wao ili tuwaone super sports wasipewe nafasi..kiwanngo kama unacho kitaonekana na kama huna/hawana kiwango waliopo team ya taifa wataonekana tu..Kama hasira yao hawawaoni wachezaji wao wakiitwa team ya taifa ina maana coach na wachezaji wake viwago vidogo..

    ReplyDelete
  2. Umeoona eeeh,sasa lawama zinakuja vip?wakati timu inacheza vizuri hata ukiangalia Nigeria waliachwa masuper stars ikawa bongo jamani? tuache majungu jamani mpira uwanjani.Kuna 1.kuna team kushinda kutokana na team work na kuna team 2.kushinda kutokana na team work pamoja na ufundi wa mchezaji mmoja mmoja nadhani Kagera wanashinda kwa ajiri ya team work ila ukiangalia mchezaji mmoja mmoja bado.

    ReplyDelete
  3. Kibadeni yuko shahihi.Kocha wa timu ya Taifa anatakiwa kufuatilia wachezaji wa timu zote badala ya kusubiri wale wanaosajiliwa na Simba ,Azam, Yanga na Mtibwa.Huku ni kutegea kwa vile anajua timu hizi tatu zinafundishwa na makocha wa kigeni na hivyo hapati shida.Mbona Maximo alikuwa anakwenda hata kwenye timu zingine na ndiko alikowapata kina Vincent Barnabas.Malegesi Mwangwa,Stephen Mwasika,Godfrey Bonny,Mwinyi Kazimoto,Shaaban Dihile,Uhuru Selemani,Jerry Tegete,Mbwana Samata,Obadiah Mungusa,Omega Seme,Thomas Ulimwengu,Saidi Morad,Adam Kingwande,Erasto Nyoni na Khamis Mcha.Wakati wa Maximo Simba,Yanga na Azam zilikuwa zinasubiri wachezaji waitwe Taifa Stars ndipo ziwasajili lakini sasa hivi kocha wa Stars anasubiri Simba,Yanga na Azam zisajili wachezaji ndipo yeye awaite

    ReplyDelete
  4. Mnnh mdau hapo juu ni vizuri tukakusaidia mawazo ya kiuanamichezo.Kibadeni pamoja na Mkwasa ni watu wenye ufahamu mkubwa wa wa soka! Wamecheza enzi zao kwa mafanikio makubwa.Pia wamekuwa kwenye kazi ya ukocha muda mrefu kwa mafanikio ndio maana wamekuwa wakikabidhiwa majukumu ama kwenye timu za taifa au timu za ligi kuu mbalimbali! Taifa lolote huwa linakuwa na watu wa namna hii! na hii ndio njia mojawapo ya wao kulisaidia taifa.Yaani kushauri.Sio kwamba hawampendi Marsh au wanataka kuingiza watoto wa timu zao tu na bila shaka Marsh na TFF watachua hilo kama changamoto kwa baadae.Timu zipo nyingi na hiyo ni timu ya Taifa.

    ReplyDelete