Search This Blog

Friday, January 10, 2014

YANGA DIMBANI KESHO DHIDI YA ANKARA SEKER SPOR.


Wakati mabingwa wa soka wa Tanzania Bara, Yanga kesho wanacheza mechi yao ya kwanza dhidi ya timu daraja la kwanza ya Ankara Seker Spor, uongozi wa timu hiyo leo utatangaza jina la kocha mkuu katika mkutano na waandishi wa habari.
Mechi hiyo itachezwa saa 9.00 za Tanzania kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Mashindano wa kimataifa wa Yanga, Seif “Magari” Ahmed amesema kuwa mazoezi ya jana yalifanyika asubuhi kutokana na jua kuwahi kuzama na hali ya hewa kubadilika.
Ahmed alisema kuwa wachezaji wanaendelea vizuri na mpaka sasa wamepania kufanya vyema katika mchezo huo ambao unatarajiwa kuwa mkali na wa kusisimua.Alisema kuwa baada ya mechi hiyo, timu hiyo itaendelea na mazoezi kabla ya kucheza mechi nyingine mbili na timu za madaraja ya juu.
“Timu imeanza kambi rasmi, na mazoezi mazuri na maandalizi yametupa moyo japo ka siku ya kwanza, kesho (leo) watacheza mechi ya kirafiki ya kwanza na timu ya daraja la kwanza, n mechi nzuri kwani timu hiyo inashika nafasi za juu katika ligi hiyo,” alisema Seif.
Alisema kuwa kwa sasa timu yao inakaa mji mwingine tofauti na Antalya ambao upo kilometa 70 kutoka mji wao wa zamani. Wamefikia hotel ya ufukweni ijulikanayo wa jina la Suino Beach Hotel and Site ambayo ina hadhi ya kimataifa.Wakati huo huo;  uongozi wa klabu hiyo kesho utamtambulisha kocha mkuu wa klabu hiyo katika mkutano maalum na waandishi wa habari makao makuu ya klabu hiyo.
Seif alisema kuwa wamepitisha majina matano na walikuwa kwenye makubaliano nao mmoja wao ambaye kesho (leo) tutamtangaza rasmi.
Alisema kuwa wamepata kocha mzuri ambaye anajua mazingira ya Afrika na anajua maisha ya mpira kwa bara hili.

No comments:

Post a Comment