Search This Blog

Friday, July 15, 2011

SAKATA LA USAJILI WA YONDANI NA TEGETE

Wakati dirisha la usajili Tanzania likiwa linafungwa leo saa 6 usiku klabu ya Simba imethibitisha kuwa wamepeleka ofa ya kutoa kiasi cha pesa pamoja na kumtoa beki Kevin Yondan ili waweze kupata saini ya mshambuliaji Jerryson Tegete kutoka Dar Young Africans.

Simba ambao leo hii pia wamefanikiwa kukamilisha usajili wa Felix Sunzu wanamhitaji Tegete aje kuziba pengo lilioachwa na mshambuliaji Mussa Hassan Mgosi anayekaribia kujiunga na DC Motema Pembe.

No comments:

Post a Comment