Search This Blog

Friday, July 15, 2011

KITABU CHENYE UMRI MKUBWA CHAPIGWA MNADA

Kitabu chenye umri mkubwa kuliko vyote cha sheria za soka ambacho kilikuwa chini ya umiliki wa Sheffield Fc kimepigwa mnada na kuuzwa kwa thamani ya paundi 881,250.
Kitabu hicho ambacho kimeandikwa kwa mkono tangu mwaka 1857 kinadhaniwa kuwa moja ya vitabu vya awali kuliko vyote vya mchezo wa soka na kimeuzwa kama sehemu ya kumbukumbu muhimu za klabu YA Sheffield Fc. Klabu hiyo imekipiga mnada kitabu hicho kama sehemu ya mpango wake wa kuchanga fedha kwa ajili ya kuendesha klabu hiyo.


HIKI NDO KIKOSI CHA KLABU KONGWE KABISA ULIMWENGUNI YA SHEFFIELD FC ILIYOANZISHWA MNAMO MWAKA 1857

Ndani ya kitabu hicho kuna sheria ambazo baadhi ziko hadi leo hii kama vile “in-direct free kick” , kona na matumiz ya sehemu ya juu ya goli maarufu kama mtambaa panya .
Sheria nyingine inaonyesha kuwa mchezaji anaruhusiwa kusukuma kwa kutumia mikono ila sio kumuangusha au kumpiga mchezaji mwenzie mweleka

HIKI NDO KITABU CHENYEWE

No comments:

Post a Comment