Search This Blog

Wednesday, July 13, 2011

MAN CITY WAMENIDHARAU SANA - ADEBAYOR



Emmanuel Adebayor amekubali kurudi katika mazoezi ya Manchester City Jumatatu, ingawa amehuzunishwa sana na taarifa aliyopewa na klabu hiyo.

Adebayor amekasirika sana na jinsi alivyoondolewa kutoka ziara ya America ya timu hiyo, Manu anahisi kudhalilishwa baada ya kupokea email akiwa mapumzikoni akiambiwa anaweza kufanya mazoezi na reserves tu na kwamba hatakuwa na nafasi katika kikosi cha kwanza.

The straiker , ambaye alikataa kuhudhuria mazoezi wiki hii, anaamini hakutendewa sawa: "Sijui nimewakosea nini.Nilipata email kutoka kwa klabu, nikiwa kwenye mapumziko akiniambia kuwa sitoweza ku-train na kikosi cha kwanza.Hili ni tusi kwangu kwa kuniambia kuwa na-fit kufanya mazoezi na reserves tu.

"Nitarudi mazoezini lakini nimejisikia kutukanwa na kukosewa heshima."

No comments:

Post a Comment