Search This Blog

Wednesday, July 13, 2011

CORINTHIANS WAGOMA KUONGEZA OFA YA TEVEZ


Manchester City wameambiwa na Corinthians: Ofa yetu kwa Tevez ndio ya mwisho chukueni au iacheni.

Ofa ya wabrazili hao ya paundi million 35 ilikataliwa na Eastlands club jana usiku.

City wanataka kupata angalau paundi million 50 na inaamnika klabu mbili za jiji la Milan zinafuatilia kwa karibu.

Raisi wa Corinthians Andre Sanchez alisema: “Ikiwa uhamisho wa Tevez hautokamilika mpaka kufikia Jumapili basi dili hili halitakuwepo mwaka huu.Tevez amekubali kusaini kwa miaka 4 na kupunguza kiwango cha mshahara kwa sababu anatamani kurudi hapa.

“Kama City wanataka paundi 50m basi atabaki England, Corinthians hatutoongeza ofa hiyo.”

No comments:

Post a Comment