Search This Blog

Friday, July 15, 2011

JUVENTUS WAINGIA KATIKA VITA YA KUMTWAA TEVEZ


Klabu ya Juventus nayo imeingia rasmi katika vita ya kutaka kumsaini Manchester City star Carlos Tevez baada ya kutuma ofa ya £45million, kwa mujibu kwa Corinthians.


City juzi walikataa ofa ya £35million kutoka kwa wakatoliki wa Brazil kwa ajili ya Carlos Tevez, lakini sasa ofa mpya iliyo mezani imeongezeka kwa £10million.

Ingawa raisi wa Corinthians Andres Sanchez amesisitiza kuwa hatoongeza ofa lakini anaamini kuwa Carlotos ana matamanio ya kurejea South America na kuwa karibu na familia yake, hivyo bado ana imani kuwa Tevez atachagua kujiunga na timu yake ya zamani.

Alisema: "Hakuna kilichobadilika, hajaamua kumuuza wala kuendelea kuwa nae.

"Wamepokea ofa ya £45m kutoka Juventus, lakini Tevez hataki kuendelea kubaki ulaya.

"Naendelea kuamini ofa niliyotuma ni nzuri, lakini inategemea na City wataamuaje.Kama ningekuwa raisi wa klabu anayochezea Tevez, basi nisingekubali kumuuza lakini kauli ya mchezaji ina uzito zaidi.Kama anataka kuondoka then ataondoka tu kwa njia yoyote.Katika soka mikataba imewekwa ili kuvunjwa."


No comments:

Post a Comment