Search This Blog

Saturday, July 16, 2011

SHAMTE ALLY: SITAKI KWENDA MORO UNITED


Siku moja baada ya dirisha la usajili kufungwa mshambuliaji wa Yanga Shamte Ally aliyepelekwa kwa mkopo Moro United amesema hataki kucheza kwenye timu hiyo ilipanda daraja msimu huu.
Shamte ambaye alitokea Kagera Sugar kabla ya kujiunga na mabingwa wa Tz amesema haweze kujiunga na Ruvu kwa sababu transfer hiyo imekwenda kinyume na mkataba wake mpya unavyoelekeza.
"Nilisaini mkataba mpya wa miaka na Yanga mwezi uliopita mara baada ya ligi kumalizika, huku ukiwa na kipengele cha probation ya miezi kadhaa, ambayo kama nikishindwa kuperform vizuri uwanjani then nitapelekwa kwa mkopo sehemu nyingine.Sasa nashangaa wakati sijaanza rasmi kuitumikia klabu naambiwa niende Moro kwa mkopo kitu ambacho ni kinyume na mkataba wangu na Yanga.
"Mimi najiamini nipo vizuri sana kimchezo na kama Yanga wangeniambia mapema kama sipo kwenye mipango ya mbele ya timu basi sasa hivi ningekuwa nimeshapata nafasi katika nyingine kubwa kama Yanga ambayo ilikuwa ikinitaka kwa udi na uvumba."-Shamte

Wakati huo huo taarifa kutoka ndani ya uongozi wa Yanga zinasema baada ya mchezaji huyo kugoma kwenda Moro, timu hiyo imeamua kufuata matakwa ya mkataba wao na Shamte, hivyo mchezaji huyo ataendelea kuitumikia Yanga msimu ujao.

No comments:

Post a Comment