Search This Blog

Thursday, October 13, 2011

MECHI YA UGANDA VS KENYA YAINGIZA MAPATO YA BILLION MOJA


Pamoja na kutofanikiwa kupata nafasi ya kushiriki katika kombe la mataifa huru ya afrika litakalofanyika mwakani, shirikisho la Soka la Uganda Fufa limesema limepata mapato ya kiasi cha zaidi ya 1bilioni za Uganda katika mechi dhidi ya Kenya iliyokuwa ya kuwania kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika kwenye uwanja wa Namboole.

Fufa imesema imepata jumla ya shilingi 1.024bilioni baada ya kutengeneza tiketi za dhahabu 610 ambazo zilikuwa zikiuzwa kwa shilingi 120,000 za Uganda, ambapo zilibaki tiketi 10 tu.

Tiketi zote 38,865 zilizokuwa zikiuzwa kwa shilingi 20,000 za Uganda ziliuzwa, lakini tiketi 503 za VIP hazikuuzwa kwa mujibu wa Fufa.

"Hatuna hizo fedha hivi sasa, tumetumia kiasi cha shilingi 561milioni za Uganda kwa mambo mbalimbali hivyo tutabakiwa na kiasi kisichozidi shilingi 500 za Uganda,"alisema Makamu wa Raisi wa Shirikisho la Soka la Uganda, Anthony Kimuli.

Alisema,"kiasi hicho cha fedha tumekitumia kwa ajili ya tiketi za kitaalamu, kambi ya timu ya Taifa, waamuzi, uwanja wa Namboole na walinzi 4,000."

Raia wengi wa Uganda walikosa tiketi za mechi hiyo ambayo ilimalizika kwa matokeo ya 0-0 dhidi ya Kenya na hivyo Uganda kushindwa kufuzu Fainali za Nataifa ya Afrika wakati ilikuwa ikishinda mechi hiyo kwa idadi yoyote ya mabao inafuzu.

Watu wengi waliopata tiketi waliweza kuzipata kwa gharama za juu kwa sababu tiketi hizo zilikuwa zikiuzwa nje ya uwanja kwa gharama ya juu.
Wakati huo huo kocha wa timu ya Taifa ya Uganda, Bobby Williamson amesema kocha yeyote angefanya uamuzi kama wake wa kumtimua kambini nyota wa timu hiyo David Obua kutokana na vitendo vyake vya utovu wa nidhamu.

"Kitu kibaya ni kwamba Obua anasema uongo, nilimtumia ujumbe wakati alipokuwa akisema uongo katika radio moja wakati akihojiwa, nilimuambia aseme ukweli ili jamii ifahamu ukweli halisi,"alisema Williamson.

Alisema,"nilijaribu kuzuia ili tusimtimue kwenye kambi, lakini vitendo vyake vya utovu wa nidhamu vilizidi huku akielewa yeye alikuwa ni mchezaji wa kuigwa na vijana wengine waliokuwa kwenye kambi ya timu ya Taifa."

Williamson alisema,"katika timu ya Taifa tunafanya kazi kitimu, lakini yeye alikuwa hataki hilo na kufanya vitendo vya utovu wa nidhamu."

Hivi sasa mashabiki wa soka nchini Uganda wanata ka kocha Williamson pamoja na Mwenyekiti wa Shirikisho la Soka la Uganda, Lawrence Mulindwa kujiuzuru baada ya kumfukuza kambini Obua saa 24 kabla ya pambano lao dhidi ya Kenya.

Baadhi ya mashabiki wa soka nchini Uganda wanaamini kukosekana kwa Obua kulisababisha Uganda kushindwa kufuzu Fainali za Afrika kwa sababu katika mechi dhidi ya Kenya timu ya Uganda ilikosa nfasi nyingi za kufunga na kujikuta wakitoka sare ya 0-0 na Kenya.

No comments:

Post a Comment