Search This Blog

Friday, July 6, 2012

YANGA WAMSAINISHA TOM SAINTIFIET KWA MIAKA MIWILI

Hatimaye siku mbili baada ya kutua nchini kocha Tom  Saintifiet kutoka nchini Ubelgiji, leo ameingia mkataba wa kuifundisha klabu ya Yanga kwa kipindi cha miaka miwili.

Akizungumza mara baada ya kuingia mkataba huo katika Makao Makuu ya klabu ya Yanga , Mwalimu huyo amesema anatarajia kufanya kazi kwa nguvu sana ili kuhakikisha Yanga inafanikiwa ndani na nje ya mipaka ya Tanzania

Saintifiet amesema Mkataba huo wa miaka miwili amesema anatarajia  kuutumia katika kuleta maendeleo katika Klabu ya Yanga ikiwemo kukuza vipaji katika soka la Vijana.
 
Naye Katibu Mkuu wa klabu ya Yanga, Mwesiga Selestine amesema Mkataba huo huenda ukawa ni endelevu iwapo uongozi utaridhishwa na mwenendo wa Kocha huyo.
 

3 comments:

  1. analamba dolari ngapi ??

    ReplyDelete
  2. Hivi shaffih zile siku 7 ulizompa akilimali hazijakwisha tu?

    ReplyDelete
  3. nigeria alikuwa nalamba $20M kwa mwezi je yanga wanampa ngapi?

    ReplyDelete