Search This Blog

Saturday, July 7, 2012

MCHAKATO WA LIGI KUENDESHWA KAMPUNI WAFIKIA ASILIMIA 95 SASA

Hatimaye mchakato wa vilabu kuweza kufungua kampuni itakayosimamia umeanza kufikia mwishoni.

Kwa taarifa nilizonazo leo kumekuwepo na kikao cha mwisho kilichokaa kwa kuwahusisha viongozi kutoka kwenye vilabu vyote vya ligi kuu ambao ndio wanaounda kampuni itayosimamia ligi kuu ya Tanzania bara msimu ujao.


Kwenye kikao hicho mambo yote muhimu katika kuelekea kwenye mchakato huo wa kuanzishwa kwa kampuni na sasa kilichobakia ifikapo wiki ijayo - viongozi hao wa vilabu watapeleka mfumo mzima na utaratibu waliopanga kwa namna ya kuendeshwa kwa ligi msimu kwa kamati ya utendaji ya shirikisho la soka kwa ajili ya kupata mawazo tofauti ili kuleta maboresho kama yatakuwepo - na mchakato wa kuifungua kampuni kuanza mara moja.

1 comment:

  1. Ni lengo zuri sana,ningewashauri wakodi kampuni ndio iendeshe ligi na kuepuka conflict of interest,tuliona kamati ya ligi chini ya mzee said na kaburu wakitoa maamuzi yasiyo yao na kuingilia kamati ya nidhamu kwa faida zao binafsi,wakigombana na mzee tibaigana alipowaambia ukweli kamati yao ya kisiasa

    ReplyDelete