Search This Blog

Saturday, July 7, 2012

FELIX SUNZU ARUDI DIMBANI NA KUIPELEKA SIMBA NUSU FAINALI YA URAFIKI CUP

Mshambuliaji wa kimataifa wa Simba na Zambia Felix Muamba Sunzu leo amerudi dimbani kuitumikia tena klabu yake ya Simba na kuifungia goli la pekee na la ushindi kwenye mchezo wa kombe la Urafiki linaloshindaniwa huko Zanzibar.

Simba imeifunga timu ya vijana ya Zanzibar Karume Boys kwa bao 1-0 liliowekwa kimiani na Mzambia huyo.

Kwa matokeo hayo Simba ambao walianza vyema michuano hiyo inayofanyika kwenye Uwanja wa Amaan mjini hapa kwa ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya mabingwa wa Zanzibar, Mafunzo kabla ya kuja kushikiliwa kwa sare ya 1-1 na Azam, ambao ni washindi wa pili wa Ligi Kuu ya Bara.

Azam FC ilimaliza ikiwa ya pili kwa kuwa na pointi 5 baada ya sare mbili na ushindi katika mechi iliyochezwa mapema jana.


Katika mechi hiyo, Azam iliilaza Mafunzo ya hapa kwa mabao 3-2.

2 comments:

  1. Shaffih ulishamalizana na mzee akilimali?au alichosema ilikuwa kweli maana ulimpa siku 7,na sijui zinakwisha lini

    ReplyDelete
  2. karibu sana sunzu watakukoma msimu huu. kila la heri katika mashindano ya kagame.

    ReplyDelete