Search This Blog

Friday, March 14, 2014

VAN PERSIE: NINA FURAHA MAN UNITED, NA NINATAKA KUENDELEA KUWA HAPA HATA BAADA YA MKATABA KUISHA."

Mshambuliaji Manchester United Robin van Persie amesema rasmi kwamba anataka kubakia Old Trafford kwa muda mrefu. 
Mwanasoka huyo mwenye umri wa miaka 30 amekanusha kwamba haelewani na kocha David Moyes na imekuwa ikisemekana kwamba angeondoka kwenye timu hiyo kipindi kijacho cha usajili.  
Lakini nahodha wa Uholanzi anasisitiza kwamba anapendelea kubakia United.
"Ukweli ni kwamba nina furaha sana," Alisema. "Nilisaini mkataba wa miaka minne na nina furaha kuendelea kukaa hapa kwa muda mrefu, hata baada ya miaka yangu miwili iliyobaki." 
Pia tetesi zimekuwa zikisema kwamba Van Persie havutiwi na mbinu za ufundishaji za Moyes. 
Lakini akiongea katika interview aliyofanyiwa na United Review, kuelekea mchezo dhidi ya mahasimu wao Liverpool, aliongelea juu ya saula la mbinu za Moyes. 
"Hakuna shaka kwamba ninajifunza mbinu mpya na ninaendelea vizuri chini ya David Moyes," alisema. "Vipindi vya mazoezi tunavyokuwa kuwa navyo ni vizuri mno na ninajifunza vitu vingi kutoka kwenye mazoezi hayo kila siku. 
"Kuna hali nzuri ya kuheshimiana baina yetu na mazingira yetu ya kufanya kazi ni mazuri. Moyes anataka sana kazi iende vizuri na mie ninataka hivyo pia."

No comments:

Post a Comment