Search This Blog

Wednesday, May 22, 2013

NGASSA ASAJILIWA BILA KUPIMWA, FEDHA ZA EL MERREIKH ZIMEMPONZA, NI HALALI KUCHEZA YANGA


LAZIMA tuamini kwamba aliyekuwa kiungo mshambuliaji wa Simba, Mrisho Ngassa amejiunga na Yanga na ataichezea timu hiyo michuano yoyote itakayoshiriki kuanzia sasa.
Ngassa amejiunga na Yanga huku kukiwa na vitimbi kadhaa vilivyotokea tangu anaondoka katika timu hiyo miaka michache iliyopita, wakati huo Yanga ilikuwa chini ya Mwenyekiti, Iman Madega.
Winga huyo aliondoka Yanga na kujiunga na Azam FC katika usajili ambao haukutarajiwa na wengi kutokana na mapenzi ya Ngassa kwa Yanga, bila shaka fedha iliongea. Azam ililipa zaidi ya Sh. 90 milioni ili kumnasa mchezaji huyo.

Mwaka jana katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, akiwa anaichezea Azam, Ngassa baada ya kuifungia bao muhimu timu hiyo katika nusu fainali, alikwenda kwenye kibendera cha kona na kukibusu. Kibendera hicho kina rangi ya kijani na njano, rangi hizo zinatumiwa na Yanga.
Hiyo ilionekana kama ishara ya kuitukuza Yanga na kuidharau Azam timu inamlipa mshahara na posho nyingine, kwa kifupi ni mwajiri wake. Azam haikupendezwa na hali hiyo, kabla ya kuanza kwa msimu huu ikatangaza kumtoa kwa mkopo kwa Simba.
Wakati Azam inatangaza kumtoa kwa mkopo au kumuuza Ngassa, nilijua fika kwamba Yanga inaweza kutia mkono wake hivyo ikatazama mazingira ya kumkwamisha kurejea katika klabu yake na kuhakikisha anakwenda Simba.
Alipokuwa Simba, Ngassa alipata ‘deal’ la kujiunga na klabu ya El Merreikh ya Sudan, viongozi wa Simba walizungumza na El Merreikh bila ya kupata ridhaa ya Ngassa. Mwisho wake mchezaji alikataa kujiungana timu hiyo ya Sudan.
Azam ambayo nayo ingefaidika kama Ngassa angejiunga na El Merreikh, ni wazi haikupendezwa na hali hiyo ya Ngassa kukataa kuiunga na klabu hiyo. Mkakati ukapangwa.

Lakini wakati haya yakitokea siku za nyuma hebu tutazame namna Ngassa alivyosajiliwa na Yanga huku kukiwa na mambo kadhaa ya kushangaza;

NGASSA HAJAPIMWA AFYA

Kama ilivyo kawaida ya timu nyingi za Tanzania, safari hii Ngassa amesajiliwa na Yanga kwa mkataba wa miaka miwili bila ya kupimwa afya…!
Jambo hili la wachezaji kusajiliwa bila kupimwa afya sasa linaonekana la kawaida ambalo klabu zimerithi utaratibu huo toka zamani, Dunia imebadilika lakini viongozi wengi wa soka hapa nchini hawatazami hili.
Kwa mfano Ngassa anaweza kuwa na matatizo ya afya katika viungo vyake vya mwili ambavyo baadaye anaweza kuigharimu klabu kumgharamia matibabu kwa mfano matatizo ya goti.
Matibabu hayo yanaweza kuigharimu klabu kiasi kikubwa cha fedha ambacho kingeweza kufidiwa wakati wa usajili wake.

FEDHA ZA EL MERREIKH ZAMPONZA
Kama inavyodaiwa kwamba, Ngassa amesaini mkataba wa mwaka mmoja wa kuitumikia Simba, baada ya deal la kumpeleka El Merreikh kushindikana, Simba na Azam ziliamua kupeleka mkataba huo wa Simba kwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ili kuusajili ili Ngassa asiwe na uamuzi mwingine atakapoamua timu ya kujiunga nayo mkataba wake utakapoisha Azam.  
Lengo la Azam na Simba lilikuwa ni kuona Ngassa hajiungi na Yanga na anaichezea Simba msimu ujao pia, HATA KAMA BILA RIDHAA YAKE.
Kwa kuwa Ngassa anafahamu anachofanya na anaheshimu maamuzi yake, aliamua kusaini kuichezea Yanga ili acheze soka kwa amani zaidi.
Usajili wa Ngassa kwa Simba (kama kweli alisaini) ulikuwa wa kama ‘kishika uchumba’ ili awe na uhakika na ahadi ya kusajiliwa na klabu hiyo, hivyo baadaye angeweza kuwa na maamuzi mengine kama alivyofanya sasa.

NGASSA NI HALALI YANGA
Kama kweli TFF itafuata hatua kwa hatua katika kile kinachoitwa mkataba wake na Simba, Ngassa ataichezea Yanga msimu ujao, kwani kuna vitu vingi vilifanyika katika mkataba huo bila ridhaa ya mchezaji.
Jambo hili linaweza kuwa kama la usajili wa Kelvin Yondani na Mbuyu Twite.

13 comments:

  1. Shaffii,Hebu angalia picha ya ngasa na Kaburu wakati anasajili yanga halafu linganisha picha ya ngasa na Mwalusako hapo juu wakati anasajiri yanga. Umegundua tofauti yoyote?

    Mwamba

    ReplyDelete
  2. amelazimishwa!mwanaume huwa hana asili ya umbea ila ww unayotabia hiyo ya kike,dhana ya kishika uchumba inatoka wapi au umezoea kuolewa,nyan wa bukoba shafi daudi kiboga

    ReplyDelete
  3. Ngasa ni mchezaji ambaye anajielewa, ana washauri wa maana na heshimu ukimshauri, hao simba na azam walindekeza uhuni sana suala la el mereikh, mtu alikuwa bado miezi 5 mkataba walitaka kuchukua miloni 160 halafu mchezaji akalipwe 78 kwa miaka miwili kwa hesabu ya milioni 5 kwa mwezi. Wakati azam kwa mshahara wa milioni 2 wanaompa kwa miezi 5 ni milioni 10 zilibaki sasa hizo 160 zilkuwa za nini, wangempa ngasa angeenda tu. Kamaliza mkataba mwacheni afanye alipendalo muda wenyewe wa kucheza unaisha mapema sana, halafu tuuuh

    ReplyDelete
  4. Fine Shafii, You may be right to a certain extent.But only problem is that it seems your analysis is too conclusive. You have shown for example that Simba and Azam submitted Ngasa's contract to TFF without his concert.The question comes how can one prove beyond doubt about non involvement of the player.The fact that he signed and took Simbas money willingly,may be used by Simba and Azam to conclude that the player was consulted before his contract was submited to TFF.If i could ask a question, do you think Ngasa's willingness/concert would change the content of the contract.One's willingness belongs to ones heart. Today you may i am willing next day you say i am not willing. But writings(contract) is for public consumption.It is out of the player's everyday decisions.In other words players are bound and should be bound with contracts and not their willingness. At one time Fabriges was an Arsenal player although his heart was residing with Barcelona.Song is now with Barcelona, although his heart might be desiring to rejoin Arsenal.There are also facts that that some players in the premier were sold or loaned to places where they were not interested.I don't think Ngasa's saga is not so different from those few examples.The problem with Tanzania,s football stakeholders do not observe the rules.Clubs and TFF normally make decisions which pleases their hearts and not otherwise. It is an high time now players and clubs should be assisted to understand and respect their rights and obligations.If Ngasa took Simba's money and signed the contract he should responsible for that.
    So my simple conclusion is that your analysis needed to be accomodative and not judge mental as it sounds.
    Thanks though for your informative role through this lovely blog.

    ReplyDelete
  5. Dogo hana mapenzi na timu wala nini? Anachoangalia ni maslahi tu! Huwezi ukamsajili mchezaji kwa pesa ndefu kama hizo alafu useme ana mapenzi! Ile hadhi ya wachezaji walioipata kwa kuwa na mapenzi na timu kama kina kina baba isaya na kina mwameja hawezi kuipata dogo.kwa sasa anacheza na saikolojia za usimba na uyanga.anajua yanga lazima waingie kichwakichwa kwa kuwa wanatakakuikomoa simba!!

    ReplyDelete
  6. Nafikiri umegundua kitu Shaffih. Jamaa wa Yanga kabla ya kufanya usajili huwa wanafanya upembuzi na uchunguzi wa kina. Hii inawasaidia sana pindi linapokuja suala kupambana kisheria na timu inayodai usajili haukufuata taratibu. Angalia mifano ya akina Kelvin Yondan, Mbuyu Twite na sasa Ngassa. Mi niliposikia Hans Pope anakanusha kama mwezi mmoja uliopita kwamba Ngassa amesajiliwa Yanga, nikajua tayari Simba tumekwisha! Maana hata kwa Yondani walikanusha hivyo hivyo. Sidhani kama kwa miaka ya hivi karibuni tunaweza kupata kikosi imara! Maana sioni watu makini pale Simba. Namkumbuka Mzee wangu Dalali (wanasema hakwenda shule lakini kwa mtazamo wangu alikuwa mtu makini sana).

    ReplyDelete
  7. Mpira wa kisasa hakuna mapenzi huyo amebugi

    ReplyDelete
  8. Ndugu Shaffih huwa nakuamini sana ila kwa hili naona kama umechemka kidogo, hivi kama kuna mkataba wa Ngassa TFF, na pia umeridhiwa na Azam, pia kama mkataba huo Ngasa kasign na unaonesha utamalizika 2014, je huoni tayari Ngasa keshajifunga hapo concert ya Ngasa zaidi ya kusign ni ipi? Pia je kwenye sharia au kanuni za TFF kuna kipengele cha kuangalia akili ya mchezaji hata kama keshasign-nadhani kwa akili ya kawaida hakuna! Hili ni tofauti na la Mbuyu Twite kwakuwa hakukuwa na mkataba halali TFF pia wa Yondani ilitumika manouvre sababu Simba walikuwa hawajausajili mpya TFF na Angetile akatumia kigezo hicho cha kutosajili kuwapa Yanga akasahu kuwa natafuta matatizo baadae sasa umesajiliwa TFF wa Ngasa Angetile atasemaje? Pia wa Yondani walisema tarehe zimekosewa je huu nao tarehe zimekosewa?
    Hapo bila unazi Yanga wameumia ila kwa Unazi Yanga watashinda na dawa ni kumburuza Ngasa mahakamani ili kukomesha utapeli

    ReplyDelete
  9. Kwanini watu wengine mnapenda kuandika kimombo wakati mada imeandikwa Kiswahili na wachangiaji waliotangulia wametumia Kiswahili?Inakera sana kwani wengine hatujui hata umezungumzia nini@

    ReplyDelete
  10. Usitushawishi tuamini hivyo sheria itafuata mkondo wake hilo jambo la muhimu.

    ReplyDelete
  11. Shaffih najua wewe ni mnazi mkubwa wa yanga,kwa vyovyote huwezi tenda haki kwa simba.Ninachoona unaandaa mazingira ili maamuzi yatakayotolewa na TFF yaibebe yanga.Your too bias

    ReplyDelete
  12. huyu jamaa kafanya hujinga na kajishushia vibaya yaan sion hata umuhimu katika timu ya taifa coz hana nidham kabisa, 4 ma side kaniboha mno,,kaniharbia hadi mood ya kwenda kuwaangalia starz 16 june, hafai kabisa, kaa chin 2lia fuata taratibu then nenda c ha2katai co kufanya usajili ili kukomoa upande fulan hakika mzimu wa simba utamtafna. cha mwisho cfahamu but my heart will b okey kama yondani angerudi simba moyo wangu unauma xana kuona yuko upande asiostail kabisa.

    ReplyDelete