Search This Blog

Friday, May 24, 2013

KUELEKEA FAINALI YA UEFA CHAMPIONS LEAGUE - RIPOTI KUTOKA JIJINI LONDON NA SHAFFIH DAUDA

Yakiwa yamebaki masaa kadhaa kabla ya fainali ya ligi ya mabingwa wa ulaya kufanyika mmoja wa waandishi wa mtandao huu Shaffih Dauda atakuwa akiripoti matukio na taarifa muhimu kuhusu mpambano huo utakawakutanisha wapinzani wa ligi ya Ujerumani Borrusia Dortmund vs Bayern Munich.

JUPP HEYNCKES - HUU NDIO MSIMU WANGU BORA KULIKO YOTE

Akiwa na miaka 68, na zaidi ya miongo hata mitatu kwenye kufundisha soka. Kocha wa FC Bayern Munchen Jupp Heynckes anafurahia msimu wake bora kabisa kwenye maisha yake ya ufundishaji soka.
Heynckes, yupo katika mwaka wake wa 3 kwenye mkataba wake na Bayern na tayari ameshaiongoza Bayern Munich kutwaa ubingwa wa Bundesliga. UEFA Champions League - ubingwa ambao Heynckes alishinda na Real Madrid CF mwaka 1998 - anaweza kushinda kwa kuifunga Bayern mbele ya Borrusia Dortmund siku ya jumamosi, wakati kuna fainali ya kombe la Ujerumani dhidi ya VfB Stuttgart inamsubiri ili kuweza kushinda treble. Itakuwa jambo la kuvutia kwa Heynckes kumuachia nafasi Josep Guardiola.
"Sijawahi kuwa na msimu kama huu, ni kitu kizuri kuwahi kunitokea kwenye maisha yangu ya soka," alisema. "Tumevunja karibia rekodi zote. Kawaida unapofunga mabao mengi pia unaruhusu mengi, lakini wachezaji kama Arjen Robben, Franck Ribéry, Mario Gomez, [Mario] Mandžukić, Thomas Müller, [Xherdan] Shaqiri, wote wameshajivunza namna kuzuia. Hilo ni jambo muhimu kwenye soka la leo.
"Fainali itakuwa ngumu ila tumejipanga kuweza kuepeukana na machungu ya msimu uliopita. Dortmund ni timu nzuri naamini fainali itakuwa mchezo wa kuvutia."

DORTMUND - KUNDI GUMU LILIWAPA HALI YA KUJIAMINI


Kama Borussia Dortmund itashinda ubingwa UEFA Champions League pale Wembley siku ya jumamosi, kwa hakika watakuwa wameshinda kwa njia ngumu.
Wakiwa wamepangwa kwenye kundi gumu lilohusisha timu zilizobeba ubingwa msimu uliopita AFC Ajax, Manchester City FC na Real Madrid CF, ambao walikuja kukutana nao kwenye nusu fainali na Robert Lewandowski akaisaidia timu yake kuidhalilisha Madrid.
Lakini mechi nyingine za kusisimua walizofanya maajabu kwa mabao ya dakika za mwisho kwenye mechi hatua ya mtoano na robo fainali dhidi ya Malaga na Shakhtar Donetsk. 
"Tumekuwa na wakati mzuri mpaka sasa kwenye michuano hii, kuanzia kwenye hatua ya makundi mpaka tulipofika fainali. Mechi za makundi zilitufungua macho na kutupa mwanga wa namna ya kupambana na vilabu bora barani ulaya na namna ya kuweza kuvishinda.
Wanaosimama mbele ya Dortmund ni washindi wa pili wa msimu uliopita FC Bayern Munich. Wanaweza wakawa wamemaliza lgi wakiongozwa kwa pointi 25 na vijana wa Jupp Heynckes na walipoteza mechi zao mbili kati ya nne za mwisho walizokutana, lakini kocha Klopp hatishwi na hali hiyo. Anasema kwamba inawezekana huu ndio ukawa mchezo mkubwa zaidi wa BVB tangu ushindi wa fainali ya UCL mwaka 1997.  

"Mpango wetu ni kuufanya huu mchezo kama mwingine, hatutaki kujipa presha, ingawa tutacheza kwa namna ya tofauti ili kuweza kujihakikishia ushindi."

No comments:

Post a Comment