Search This Blog

Thursday, November 10, 2011

BREAKING NEWZ: TENGA KUKUTANA NA VIONGOZI WA VILABU VYA LIGI KUU KESHO


Sekeseke kati ya vilabu vya ligi kuu na shirikisho la soka nchini linatarajiwa kuchukua sura mpya hapo kesho baada ya Raisi wa shirikisho hilo, Leodgar Tenga kuwaita viongozi wote wa vilabu vinavyoshiriki katika ligi kuu kukaa katika meza moja na kujadili juu ya mustakabali wa namna ya kuiendesha ligi.

Mkutano wa Tenga na viongozi wa vilabu unatarajiwa kufanyika kesho katika makao makuu ya TFF-Karume stadium jijini Dar es Salaam.

Madhumuni yanatarajiwa kuwa ni kujadili juu mgogoro unaoendelea kati vilabu na TFF kuhusu namna gani inayofaa kuiendesha ligi kuu ya TZ bara msimu ujao.

Kwa muda mrefu sasa viongozi wa vilabu wamekuwa wakisema kuwa msimu ujao watachukua majukumu ya kuendesha ligi kupitia kampuni yao itakayoundwa na vilabu vishiriki, wakati TFF wakiwa wanataka ligi kuu iendeshwe kupitia kamati ya ligi.

1 comment:

  1. TFF wameamua kitu cha maana sana kukutana na uongozi huo wa vilabu,tunachotaka ni kuona ligi ikiendeshwa na kampuni na si vinginevyo,nawaomba tff waelewe msimamo wa vilabu ni kwa faida ya wote,KENY MGAYA from Arusha.

    ReplyDelete