Search This Blog

Thursday, November 10, 2011

TAIFA STARS YAWASILI SALAMA CHAD


Taifa Stars imewasili jana usiku hapa N'Djamena tayari kwa mechi ya kwanza ya mchujo ya Kombe la Dunia dhidi ya Chad itakayochezwa kesho Uwanja wa Idriss Mahamat Ouya.

Timu imefikia hoteli ya Santana, na leo saa 10 jioni kwa saa za hapa itafanya mazoezi ya mwisho Uwanja wa Idriss Mahamat Ouya. Kesho mechi itaanza saa 10 kamili jioni ambayo kwa nyumbani ni saa 12 jioni.

Wachezaji wote wako katika hali nzuri isipokuwa beki Erasto Nyoni ambaye ameamka leo asubuhi akiwa na malaria. Kocha Jan Poulsen amesema atatangaza kikosi kitakachoanza mechi ya kesho baada ya mazoezi ya leo jioni.

Waamuzi wote wanatoka Nigeria. Mwamuzi wa kati atakuwa Bunmi Ogunkolade wakati wasaidizi ni Tunde Abidoye na Abel Baba. Kamishna wa mechi ni Hamid Haddadj kutoka Algeria.

Stars imekuja hapa na kikosi cha wachezaji 21 ambacho kitarejea nyumbani siku moja baada ya mechi kwa ndege ya Ethiopian Airlines kwa kupitia Addis Ababa, Ethiopia. Timu itawasili Novemba 13 mwaka huu saa 7.25 mchana na kwenda moja kwa moja kambini.

No comments:

Post a Comment