Search This Blog

Wednesday, November 9, 2011

JERRY SANTO ATOA SHUKRANI, APATA TIMU ULAYA, KUJIUNGA NAYO JANUARY


Kiungo wa kimataifa wa Kenya na mchezaji wa zamani wa klabu ya Simba, Jerry Santo ameongea exclusively na blog hii kuwashukuru watanzania na wapenzi wa soka hapa nchini kwa kumpa ushirikiano na kumuonyesha mapenzi kwa muda wote aliokuwa akicheza hapa Tzee.


Pia Santo ambaye aliichezea Simba katika mzunguko wa kwanza wa ligi kuu ya Tz Bara msimu huu amesema tayari ameshapata timu ya kuichezea barani ulaya inayoshiriki katika ligi kuu ya nchini Albania iitwayo KF Tirana.


Santo anasema anategemea kujiunga na timu hiyo mwezi January mwakani na anategemea kusaini mkataba wa miaka miwili wa kuitumikia klabu hiyo ambayo wakenya wenzie Moses Arita na James Situma.


KF Tirana ni moja ya timu zenye mafanikio makubwa nchini Albania.



1 comment:

  1. Tunashukuru kwa mchango wake pia kwa ameonyesha yeye ni professional wa ukweli na tunamtakia mafanikio mema huko aendako....

    ReplyDelete