Search This Blog

Thursday, November 10, 2011

NEYMAR AZITOLEA NJE BARCA NA REAL - ASAINI MKATABA MPYA

Mshambuliaji kinda wa kibrazil Neymar amesaini mkataba mpya na klabu yake ya Santos na kumaliza uvumi wa miezi kadhaa kuwa alikuwa akijiandaa kujiunga na aidha Real Madrid au Barcelona.

Baada ya wiki iliyopita kutoka kwa taarifa kuwa Neymar atajiunga na Madrid katika uhamisho wa dirisha dogo mwezi January mwakani, leo hii imedhihirika kuwa Neymar amekubali kuuboresha mkataba wake na mabingwa wa uchampioni wa Copa Libertadores.

Mkataba wa Neymar ambao unaishia 2015, utaendelea kama ulivyo lakini mbrazili huyo ameongezea kiasi kikubwa katika mshahara wake aliokuwa analipwa kwa wiki.

Wakala wa mchezaji huyo Wagner Ribeiro amethibitisha kuwa makubaliano yamefanyika na kwamba mteja wake alikuwa na furaha sasa kuendelea kubaki Santos.

“Neymar ana furaha sana kuweza kuendelea kubaki hapa mpaka 2014 baada ya World Cup, baada ya hapo labda anaweza kufikiria kuondoka.” Alisema Wagner.

Mbrazili huyo anategemea kuvuna mshahara £1.1 million kwa mwezi na thamni yake inategemea kupanda kutoka £35.7m mpaka atleast £45million.

No comments:

Post a Comment