Search This Blog

Thursday, November 10, 2011

TENGA AOMBA MIAK 4 MINGINE YA UONGOZI CECAFA ILI AMALIZE KAZI


Publish Post

Raisi wa shirikisho la soka nchini (TFF) na mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Soka kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), Leodegar Tenga amesema atagombea tena kuliongoza Baraza hilo na kwamba miaka minne mingine itamtosha kuweza kumalizia yale anayoyaona bado katika kuendeleza soka la ukanda huu.

Tenga alisema hayo jana alipokuwa akizungumzia uchaguzi mkuu wa baraza hilo unaotarajiwa kufanyika Novemba 24, siku moja kabla ya kuanza kwa mashindano ya Kombe la Chalenji,

Dar es Salaam.


Tenga, anayetetea nafasi yake atapambana na Makamu Mwenyekiti wake, Faoul Hussein kutoka Djibout, alisema kwamba dhamira yake ilimtuma kuomba miaka minne mingine ya

kulitumikia baraza hilo.


“Mimi ni muumini wa vipindi, nadhani nikipata miaka minne zaidi itanitosha,” alisema Tenga ambaye aliweka bayana kuwa hana nia ya kugombea tena baada ya kipindi cha miaka minne

mingine kuisha.


Tenga alisema kwamba haamini juu ya kukaa madarakani muda mrefu mpaka watu wanakuchoka na kuamua kukuondoa kwa aibu.


Alisema wapo watu wengi wenye uwezo wa kuongoza hivyo ni muhimu kwa kiongozi kuongoza kwa mtindo ya kuachiana madaraka.


Aliongeza kama atachaguliwa kwa miaka minne inayokuja baada ya kipindi hicho kuisha hatogombea tena na kwamba ataendelea kuchangia mawazo yake kama mwanamichezo yeyote yule katika maendeleo ya mpira wa miguu.


Kuhusiana na mpinzani wake, Tenga alisema ni haki ya kila mtu kikatiba kugombea kwa nafasi yoyote kama akipata ridhaa ya chama cha soka cha nchi yake.


Alisema yeye binafsi amepata ridhaa ya Shirikisho la Soka nchini TFF na ndio maana anagombea tena kutetea nafasi yake.

No comments:

Post a Comment