Search This Blog

Saturday, November 12, 2011

TFF YAWAPA ONYO LA MWISHO RAGE NA SENDEU


Kamati ya Nidhamu na Usuluhishi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), imetoa onyo la mwisho kwa Mwenyekiti wa Simba Ismail Aden Rage na Ofisa Habari wa Yanga Louis Sendeu kutokana na kutohudhuria vikao viwili mfululizo kama walivyotakiwa na kamati hiyo.

Rage na Sendeu wanatakiwa kujieleza mbele ya kamati hiyo iliyo chini ya Kamishna mstaafu wa Polisi, (CP), Alfred Tibaigana, kutokana na tuhuma za utovu wa nidhamu baada ya kudaiwa kutoa kauli zenye lengo la kushusha maendeleo ya soka hapa nchini, wakati wa kuelekea mechi ya Ngao ya Hisani, kati ya Simba na Yanga.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura, kamati hiyo inatarajiwa kukaa hivi karibuni ambapo imeagiza Rage ataarifiwe kuwa anayepanga vikao vya kamati hiyo sio yeye, hivyo endapo hatatokea siku atakayoitwa, atajadiliwa na mamuzi kutolewa.

Alisema Rage amekosa mara mbili kuhudhuria kikao cha kamati hiyo, hivyo kitakapoitishwa itakuwa ni mara ya tatu, hivyo kutakuwa hakuna samahani.

Septemba 24, mwaka huu, Sendeu alihojiwa na kamati hiyo kutokana na tuhuma nyingine za kutoa matamshi yenye kuhatarisha maisha ya mwamuzi Alex Mahagi, na kuhukumiwa kulipa faini ya sh 500,000.

1 comment:

  1. Hawa jamaa wameshindwa kuendeleza mpira wa nchi hii na wamegeuka mahakama.Kila siku kuamua kesi zisizo na miguu wala kichwa.Inasikitisha sana.

    ReplyDelete