Search This Blog

Friday, November 11, 2011

VAN DER SAR: SAFU YA KIUNGO YA UNITED IIMARISHWE.


Edwin van der Sar anaamini safu ya kiungo ya Manchester United inabidi iboreshwe kama klabu hiyo inataka kushindana na Barcelona msimu huu.

Mholanzi huyo ambaye alicheza mechi ya mwisho mwezi May katika mechi ambayo vijana wa Sir Alex Ferguson waliadhiriwa na kipigo cha 3-1 katika fainali ya Champions league na vijana wa Pep Guardiola.

Hata Ferguson alikiri kuwa ilikuwa mechi ya upande mmoja, huku Barcelona wakipiga pasi 662 dhidi ya 301 za United. Hali inayomfanya Van Der Sar aamini mabingwa wa England wajaribu kubadilisha mfumo wa uchezaji wao hasa katika safu ya kiungo kama wanataka kufanikiwa barani ulaya msimu huu.

No comments:

Post a Comment