Search This Blog

Saturday, January 14, 2012

GARY CAHILI KUTAMBULISHWA LEO STAMFORD BRIDGE



Chelsea wamekamilisha usajili wa beki Gary Cahil lakini hatoweza kucheza leo dhidi ya Sunderland in premier league clash katika uwanja wa Stamford Bridge.


Cahil jana alikubaliana na mahitaji binafsi ya kupata mshahara wa £80,000 kwa wiki kwa mkataba wa miaka 5 na anatarajiwa kusafiri kwenda London kwa ajili ya kufanyiwa vipimo vya afya leo jumamosi.


The Blues walikuwa na matumaini ya kukamilisha uhamisho wa Cahil mapema jana mchana ili aweze kucheza mechi ya leo dhidi ya Black Cats, lakini haikuwezekana hivyo leo baada ya kufanyiwa vipimo, Gary Cahil atatambulishwa rasmi kwa mashabiki kabla ya mchezo huo.


Ni zaidi ya wiki mbili sasa tangu Bolton wakubali ada ya uhamisho ya £7million kutoka kwa Chelsea kwa ajili ya Cahil, ambaye alikuwa katika miezi 6 ya mwisho ya mkataba wake.


Mazungumzo kati ya Chelsea na mchezaji ndio yalikwamisha uhamisho huo kukamilika mapema, huku Andre-Villas Boas akisema mahitaji makubwa ya mshahara ndio kikwazo.


Inaaminika Cahil alikuwa akitaka alipwe kiasi cha £100,000 per week, £30000 zaidi ya kiasi ambacho Chelsea walikuwa wapo tayari kulipa, wakiwa katika program ya kupunguza matumizi makubwa yatokanayo na mishahara ya wachezaji .


No comments:

Post a Comment