Search This Blog

Friday, January 13, 2012

TWIGA STARS UWANJANI KESHO

Timu ya Taifa ya wanawake (Twiga Stars) kesho (Januari 14 mwaka huu) inacheza na wenyeji Namibia katika mechi ya kwanza kuwania kufuzu kwa fainali za Afrika kwa Wanawake (AWC) itakayofanyika Uwanja wa Sam Nujoma jijini Windhoek kuanza saa 12 jioni kwa saa za Afrika Mashariki. Twiga Stars iliwasili salama jijini Windhoek jana (Januari 12 mwaka huu) saa 4 asubuhi kwa ndege ya Air Namibia ikitokea Johannesburg ambapo imefikia Safari Hotel. Baada ya mapumziko jana jioni ilifanya mazoezi.Leo jioni (Januari 13 mwaka huu) imefanya mazoezi kwenye Uwanja wa Sam Nujoma ambapo ndipo mechi itachezwa kesho. Hali ya hewa ya Windhoek ni baridi kidogo kulinganisha na Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment