Search This Blog

Wednesday, September 28, 2011

BREAKING NEWZ: MAN CITY YAMSIMAMISHA CARLOS TEVEZ


Klabu ya Manchester City imemsimamisha mshambuliaji wake Carlos Tevez baada ya kukataa kuingia uwanjani kama sub katika ya jana dhidi ya Bayern Munich.

Taarifa rasmi ya klabu ilisema:

“Manchester City inathibitisha kwamba mshambuliaji Carlos Tevez amesimamishwa mpaka hapo itapotolewa taarifa nyingine katika kipindi kisichopungua wiki mbili.

“Kusimamishwa huku kwa Tevez kunafuatia madai ya vitendo alivyovifanya wakati wa mchezo wa Jumanne tuliofungwa 2-0 na Bayern Munic.

“Mchezaji hatoruhusiwa kushiriki katika mechi wala mazoezi wakati wote wa adhabu.”

2 comments:

  1. Sidhani kama ni sahihi kwa Mancini kumuweka benchi striker wa 20+ goals a season. Pia kusajili mastriker wapya Dzeko na Aguero ni dhahiri Mancini hamhitaji Tevez, ila inashangaza kwanini hakufanya juhudi za makubaliano ya mauzo? Inakuwa kama anamkomoa vile.
    Lakini bado nabaki nikiamini kuwa mastriker wote wa Man City hakuna jembe kama Tevez.Huyu jamaa atahama, sijui Arsenal wangeweza jamaa angeonesha makali yake haswa.

    ReplyDelete
  2. nadhani tevez alitaka kuondoka tangu siku nyingi ila hakuweza sasa ameamua kuonyesha vimbwanga. hayo ndo kama yale ya robihno na hizi mbwembwe zinaweza kuua timu

    ReplyDelete