Search This Blog

Thursday, April 25, 2013

DORTMUND 4-1 MADRID: LEWANDOSKI AWA MCHEZAJI WA KWANZA KUIFUNGA MADRID MABAO MANNE KWENYE HISTORIA YA CHAMPIONS LEAGUE - CRISTIANO RONALDO AWEKA REKODI 2 BINAFSI

Dortmund* Mshambuliaji wa Dortmund Robert Lewandowski ndio mchezaji wa kwanza kufunga mabao manne dhidi ya Real Madrid katika historia ya ligi ya mabingwa wa ulaya.

* Ilikuwa ni mara ya 10 kwa mchezaji mmoja kufunga mabao zaidi ya manne katika mechi moja ya Champions League. Lionel Messi pekee ndio mchezaji aliyefunga mabao manne mara mbili katika mechi 2 za ligi ya mabingwa wa ulaya.

* Huu ndio msimu wa kwanza ambapo timu zimeruhusu nyavu zao kuguswa mara 4 katika mechi za hatua ya kutoana kwenye ligi ya mabingwa wa ulaya. Bayern 4-0 Barcelona, Dortmund 4-1 Real Madrid.

* Cristiano Ronaldo nae ameweka rekodi ya kuwa mchezaji wa 3 kufunga kwenye mechi sita mfululizo za ligi ya mabingwa ulaya, wengine waliofanya hivyo ni Chamakh na Burak Yilmaz.

* Ronaldo amekuwa mchezaji wa tano kuweka rekodi ya kufikisha mabao 50 ya Champions League. Akiwafuatia Raul 71, Lionel Messi 59, Ruud van Nistelrooy 56 and Thierry Henry 50.

* Timu pekee iliyowahi kugeuza matokeo baada ya kufungwa 4-1 katika mchezo wa kutoana wa Champions League ni Deportivo La Coruna ambao walifungwa 4-1 na AC Milan katika mechi ya kwanza jijini Milan lakini wakaenda kushinda 4-0 kwao Hispania.

* Katika historia michuano ya ulaya ya klabu kumekuwepo na fainali moja tu iliyowakutanisha timu kutoka Ujerumani. 1979-80 UEFA Cup, Frankfurt wakiwafunga Borussia Moenchengladbach.

3 comments:

  1. FIFA wana kp cha kutuambia kupitia data chache km hizi?
    1. Ligi bora-Laliga
    2. Mchezaji bora-Laliga
    3. Timu yao wachezaji wote-Laliga
    4. Kocha bora-spain

    UDHAIFU:
    La liga ina ushindani kwa timu mbili tu kwa zaidi ya miaka 10 sasa, hii imetokana na utofauti mkubwa wa mapato baina ya timu mbili kubwa na timu zingne zczo na kipato kikubwa, hata hivyo FIFA wameziba mackio na kujitoa akili kwa kuiona ndio ligi bora.
    Hata chelsea waliochukua ubingwa wa UEFA japo ilikuwa kwa kubahatisha hawakutoa mchezaji yeyote kwenye kikosi cha FIFA matokeo yake mtu km Pique ambaye cjawahi kuukubali uwezo wake aliingizwa licha ya kutocheza kwa muda mrefu kutokana na kutoelewana na aliyekuwa kocha wake Pep Gudiola hivyo FIFA walimuingiza kwenye timu yao labda kwa kumtia ujauzito Shakira!
    Vivyo hivyo timu za La Liga ht fainali ya UEFA hazkucheza bt bado zkaendelea kuhesabika bora. MWISHO: TIMU YA FIFA imepigwa 8-1 na timu ambayo ligi yake huingiza timu 3 tu kwenye UEFA.
    Inackitisha sana, maghumashi hadi kwenye fani ipendwayo na wali0wengu wote!
    Majaliwa Mayala wa Buswelu Mwanza Tanzania, naishi kwa mkopo Dodoma

    ReplyDelete
  2. Sioni kinachowafanya watu mpige kelele kuhusu la liga mpende msipende La liga ni bora na Barca na Real watacheza fainali !
    HALA MADRID

    ReplyDelete
  3. Fainali pekee ambayo ingewakutanisha ni kombe la mfalme bt kwasasa labda kwa kuchezea mikono!

    ReplyDelete