
Simba ambayo imechemka kutetea taji lake la ubingwa wa ligi msimu huu, Alhamisi itakuwa kwenye kibarua kigumu kuvaana na Maafande hao, Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Mkwasa alisema jijini Dar es Salaam kuwa vijana wake wamefanya maandalizi ya kutosha kwa ajili ya mchezo huo na kuahidi ushindi.
"Tumepata muda mzuri wakujiandaa na mchezo wa Simba. Pia, hali za wachezaji wangu wote ni wazima wa afya."
"Simba ni timu nzuri, nimewaona wakicheza katika mechi tofauti. Wana vijana wenye kasi na uzoefu na ligi."
"Lakini kwetu hilo haliwezi kututisha na kucheza bila malengo ya ushindi." alisema Mkwasa ambaye alijiuzulu kukinoa kikosi cha timu ya Taifa ya Wanawake Twiga Stars.
Kocha huyo alieleza kuwa mchezo huo utakuwa mkali na wenye ushindani kutokana na timu zote mbili kuundwa na vijana wenye vipaji vya soka na kasi uwanjani.
Simba inashika nafasi ya nne kwenye msimamo na pointi 37 wakati Ruvu akiwa na pointi 30 na kukamata nafasi ya saba kwenye msimamo huku kila moja ikiwa na michezo mitatu mkononi.
No comments:
Post a Comment