Search This Blog

Tuesday, April 23, 2013

MAGUMASHI DOT COM : JKT RUVU KWA STAILI HII KWANINI WASISHUKE DARAJA ?

Zingatia tofauti za wazi zinazoonekana kwenye orodha ya watu wanaopaswa kuwepo kwenye benchi la ufundi la timu za Yanga na Jkt Ruvu. Kwa upande wa Yanga kila kitu kiko wazi kocha amewekwa,wasaidizi wake na kila mmoja amekaa kwenye nafasi yake kama inavyostahili kwenye timu inayoshiriki ligi kuu ya soka . Upande wa Ruvu Jkt kuna walakini mkubwa . Kila mmoja anafahamu kuwa kuna sheria inayozibana timu za ligi kuwa na watu wenye sifa fulani zinazohitajika kwa kocha mkuu wa timu ya Ligi kuu . Azish Kondo hana hizo sifa. Jina la Keneddy Mwaisabula limeandikwa kwa kalamu na sio kuchapishwa kama upande wa Yanga. Kennedy Mwaisabula hakuwepo uwanjani siku hiyo wakati Ruvu walipocheza na Yanga , na sababu kubwa ya jina lake kuandikwa kwa kalamu ni ukweli kwamba Ruvu walijaza jina lake ili watimize kanuni ya TFF inayohitaji makocha wenye vigezo ambavyo Azish Kondo hana. Kwa mwenendo huu Ruvu wakishuka daraja watamlaumu nani?

3 comments:

  1. kwa mtindo huu ndugu zangu hawana bahati

    ReplyDelete
  2. hii ndio bongo unauziwa cheni bandia ukiwa mjanja toa hela bandia

    ReplyDelete
  3. Je Mwaisabula ana mkataba na tim,u hiyo au deiwaka?anaruhusiwa kwenye bench bila mkataba au jina lake liliwekwa boya tu?

    ReplyDelete