Search This Blog

Friday, April 26, 2013

HATIMAYE YANGA YATAWAZWA KUWA MABINGWA WA VODACOM PREMIER LEAGUE 2012/12

Mabingwa wa Afrika mashariki na kati klabu ya YANGA leo imetawazwa rasmi kuwa bingwa wa ligi kuu ya Tanzania katika msimu wa 2012/13. 

Yanga imefanikiwa kutangaza ubingwa huo huku ikiwa imebakiwa na michezo na michezo miwili baada ya Azam FC ambao wanashika nafasi ya pili kutoka sare ya 1-1 na Coastal Union leo hii katika dimba la uwanja wa Mkwakwani.
  
Matokeo hayo yanamaanisha, Azam FC ambao walikuwa wakiikimbiza Yanga kwa karibu katika mbio za ubingwa, hawawezi kuzifikia pointi za Yanga yenye pointi 56, huku Azam ambao wamebakiwa na michezo miwili vilevile wakiwa na pointi 48 - hivyo hata wakishinda mechi zao zilizobakia watakuwa na pointi na poinri 54.

MSIMAMO WA LIGI ULIVYO HIVI SASA

                                    P W D L GF GA GD Pts
1 Yanga SC        24 17 5 2 44 13 31 56
2 Azam FC          24 14 5 5 42 20 22 48
3 Kagera Sugar   23 11 7 5 25 18 7 40
4 Simba SC         22 9 9 4 32 21 11 36
5 Mtibwa Sugar   24 9 9 6 27 23 4 36
6 Coastal Union   24 8 10 6 24 21 3 34
7 Ruvu Shooting  22 8 6 8 21 21 0 30
8 JKT Oljoro 24 7 7 10 22 27 -5 28
9 Prisons            24 6 8 10 14 21 -7 26
10 JKT Ruvu 24 7 5 12 20 37 -17 26
11 Mgambo JKT   23 7 4 12 16 23 -7 25
12 Toto African     25 4 10 11 22 34 -12 22
13 Polisi Moro      23 3 10 10 12 22 -10 19
14 African Lyon 24 5 4 15 16 36 -20 19
 

3 comments:

  1. Yanga daima mbele nyuma mwiko, mipango kimataifa zaidi tucridhike na hizi milioni 40 za ligi yetu tu. Mbona Azam wanafanya poa tu, Yanga kikosi kiko bomba sana xo cdhan km itakuwa kusajili wachezaji wengi kupita mahtaji, Brandts aachwe afanye usajili kwa kuzingatia mahtaji c kufurahisha washangiliaji.

    ReplyDelete
  2. pongezi kwa viongozi, benchi la ufundi, wachezaji, na mashabiki kwa sapoti mpka timu yetu imebeba ndoo! mdau wa yanga toka st john university of tanzania dodoma

    ReplyDelete
  3. Sasa kama wamekunya kwanini wasitawazwe?!

    ReplyDelete