Search This Blog

Thursday, April 25, 2013

ZAHA: MIE NI SHABIKI WA DAMU WA ARSENAL ILA UNITED NI KLABU KUBWA NA BORA DUNIANI SIKUWEZA KUKATAA KUJIUNGA NAYO


WILFRIED ZAHA hakuweza kukataa uhamisho wa £15million kwenda  Manchester United — japokuwa ni mshabiki wa damu wa klabu ya Arsenal.

Winga huyo ambaye anachezea Crystal Palace kwa mkopo, ni mshabiki wa tangu utotoni wa Gunners, na alikuwa na ndoto na kujiunga na Arsenal kabla ya United hawajaingia katika mbio za kumsaini.

Zaha, 20, alisajiliwa na United mwezi January kabla ya kurudishwa Palace kwa mkopo.

Winga huyo alisema: “Siku zote ilikuwa ni Arsenal, Arsenal, Arsenal, Arsenal katika kuchagua timu ambayo ningejiunga nayo.

“Siku zote nimekuwa mshabiki wa Arsenal. Sikudhani kama United watakuja kunihitaji lakini ikawa vinginevyo. Arsenal ni timu nzuri lakini United ni moja ya klabu kubwa sana duniani ilinibidi nijiunge nayo.

1 comment:

  1. Kwa kauli ya Zaha ingekuwa Bongo hasa kwa Vilabu vikongwe angesugua bench au kuuzwa bila hata mchezaji mwenyewe kujua hata kwa mkopo ili mradi tu asicheze kwenye klub hiyo. Upuuzi huu hutausikia kwa zenye weledi mkubwa kama Man U, Angalia kilichomkuta Mrisho Ngasa kulazimishwa kuondoka Azam kisa mapenzi binafsi kwa Yanga na si ajabu ukasikia Ngasa yuko Yanga msimu ujao. Sidhani kama itakuwa ni mpango wa kocha Ernest Brandist ikizingatiwa kuna damu changa ambaye yuko juu sana kushinda hata Ngasa naye ni Msuva na Luhende ktk nafasi ya wings. Mkinga C.J wa Kimara DSM

    ReplyDelete