Search This Blog

Friday, September 6, 2013

UONGOZI WA YANGA WAWAJIBU AKINA MZEE AKILIMALI - MWALUSAKO KUENDELA KUWA KATIBU MKUU WA YANGA

Makamu mwenyekiti wa klabu ya Yanga, Clement Sanga (katikati) akiongea na waandishi wa habari , kulia ni Mohamed Bhinda (mjumbe wa kamati ya utendaji) , kushoto Baraka Kizuguto Afisa Habari






Makamu mwenyekiti wa klabu ya Young Africans Clement Sanga leo amefanya mkutano na waandishi wa habari kutoa ufafanuzi juu ya habari zilizokuwa zimeenea kuhusiana na taarifa za mabadiliko ya kaimu katibu mkuu Lawrence Mwalusako kuondolewa kwenye nafasi yake na kuchukukuliwa na mtu mwingine.

Akiongea na waandishi wa habari Sanga amesema taarifa hizo hazina ukweli kwamba tayari kuna mtu anachukua nafasi ya Mwalusako, bali kilichotokea ni kutokuwepo kwa mawasiliano mazuri katika suala hilo kati ya viongozi na wazee.

Kilichopo ni kwamba uongozi wa klabu ya Young Africans upo katika mchakato wa kuhakikisha unajaza nafasi zilizopo wazi za mkurugenzi wa ufundi, mkurugenzi wa masoko, mkurugenzi wa fedha na zoezi hilo linaendeshwa na kampuni moja ambayo waliipa nafasi ya kuendesha zoezi hilo.

Zoezi likiwa ndani ya mchakato mmoja wa waombaji wa nafasi hizo Patrick Naggi aliwasili makao makuu ya klabu ya Yanga kwa lengo la kutaka kujua mazingira ya ufanyaji kazi yakoje na kufahamu baadhi ya mambo kuhusiana na klabu ndipo kulipotokea kutokuelewana na baadi ya wanachama wakiwemo wazee waliokuwepo eneo la klabu.

Kwa maana hiyo napenda kutoa taarifa kwa umma na wanachama wa Yanga kuwa uongozi bado haujatoa baraka za ajira kwa mtu yoyote katika nafasi hizo, isipokuwa ni muombaji aliwahi kufika makao makuu kabla ya mchakatao wa usahili kukamilika.

Lawrence Mwalusako anaendelea kuwa kaimu katibu mkuu wa Yanga mpaka hapo kutakapokuwa na taarifa nyingine zozote za mabadiliko kwa nafasi zote zilizopo wazi katika idara mbalimbali.
Uongozi unawaaomba wanachama, wapenzi na washabiki wa soka kuwa kitu kimoja katika kuunga mkono harakati za kimaendeleo ili kuifanya timu iende katika hatua nyingine ya ushindani wa kimatifa.

4 comments:

  1. kweli akili kumkichwa!watu ni ma critical thinker..kweli u guys r xo smart.??eti kuangalia mazingira ya kazi ndo aombe!mmmmh;dats great

    ReplyDelete
  2. hatuwezi kuendelea kimichezo kama tutakuwa na watu wanaojiita wazee wa yanga maana sijaona hata siku moja kwa club kama villa sport ya uganda au gormahia ya kenya au supersport ya africa kusini eti management inamchagua katibu mkuu afu wazee wa club wanapinga sababu eti sio mwanachama!!!
    Nakumbuka kuna sehemu nimewahi kusoma makala fulani ya rafiki yangu eddo kumwembe amewahi kuandika siku yanga na simba zikifa kuna watu wataumbuka mjini nikawa najiuliza kwa nini?? sasa nimepata majibu wakati viongozi wanawaza club itakuaje na mipango imara na bora wazee wanawaza watanufaika vp na yanga yao!!!

    ReplyDelete
  3. YANGA BILA WAZEE INAWEZEKANAAAA!!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  4. Kwani hawa wazee faida yao kwenye timu ni ipi?

    ReplyDelete