Search This Blog

Wednesday, February 15, 2012

NANI NA WELBECK NUSURA WAACHWE NA NDEGE - UNITED WAKIELEKEA UHOLANZI




Nani na Welbeck wakiwa wanachoma mahindi uwanja wa Taifa.
Kituko kimetokea leo hii jijini Manchester baada ya mastaa wawili wa Manchester United Luis Nani na Danny Welbeck walishindwa kusafiri na timu yao baada ya kusahau passport zao.

Nani na Welbeck  hata hivyo walibaki uwanjani kwa msaa kadhaa kabla ya hawajafanikiwa kujiunga na wachezaji wenzao waliokuwa wakiwacheka mno.
Kikosi cha wachezaji 20 cha United kimesafiri kuelekea Holland kwa ajili ya mchezo wa Europa League dhidi ya Ajax.
De Gea na Rooney wakiwa wenzao.



Hii itakuwa mechi ya kwanza ya United kucheza nje ya Champions league  tangu walipofungwa na Rotor Volgograd ya Russia katika round ya kwanza ya UEFA Cup in 1995.

Nani na Phil Jones wamerudi katika kikosi cha kwanza cha United baada ya majeruhi, wachezaji wengine waliokuwa majeruhi na walikuwepo katika msafara huo ni Tom Cleverley, Ashley Young pamoja na makinda Paul Pogba na Zeki Fryers.

No comments:

Post a Comment