Search This Blog

Thursday, February 16, 2012

ZAMBIA WAENDELEA KUVUNJA REKODI - WAPANDA KWA NAFASI 28 KATIKA RANKING ZA FIFA HUKU IVORY COAST WAKISHIKA USUKANI AFRICA.



Zambia wameweka rekodi nyingine siku chache baada ya kunyakua ubingwa wa kwanza wa wa AFCON,  baada ya kuvuka nafasi 28 katika rankings za FIFA ikiwa ni mara yao ya kwanza kuingia hata katika top 50 ndani ya kipindi cha miaka 11.

The Copper  Bullets waliruka mpaka nafasi ya 43, nafasi yao ya juu zaidi tangu February 2001, baada ya kuwafunga Ivory Coast kwa mikwaju ya penati mjini Libreville.
Pamoja na kupoteza nafasi ya kuchukua ubingwa, Ivory Coast wamepanda kwa nafasi 3 mpaka ya 15 na ikiwa ndio timu iliyoshika nafasi ya juu zaidi barani Afrika. Tembo hao wa Afrika hawakuruhusu nyavu zao kuguswa katika dakika za kawaida katika mashindano yaliyoisha jumamosi.

Mali, ambao walishika nafasi ya tatu, walisogea mbele kwa nafasi 25 na wakashika nafasi ya 44.

Mataifa mengine kama wenyeji Equatorial Guinea timu ambayo iliundwa na wachezaji wengi wanaocheza ligi za madaraja ya chini nchini Spain waliruka kutoka nafasi ya 151 mpaka ya 110 baada ya kufanikiwa kuingia robo fainali.

FIFA RANKINGS: TOP 10

1 Spain    
2 Germany    
3 Netherlands    
4 Uruguay    
5 England    
6 Portugal    
7 Brazil    
8 Italy    
9 Croatia    
10 Denmark

Wakati huo huo Spain waliendelea kuongoza kwa kuwa nafasi ya kwanza, wakifuatiwa na Ujerumani waliowashusha Uholanzi walioshika nafasi ya 3, Uruguay wameshika nafasi ya 4 wakifuatia na England waliofunga dimba la top 5.

No comments:

Post a Comment