Search This Blog

Saturday, December 14, 2013

BAADA YA KUUMIA - HIZI NDIO MECHI 8 ATAKAZOZIKOSA ROBIN VAN PERSIE

Mshambuliaji wa Manchester United Robin van Persie atakosekana katika kikosi cha Manchester United kwa mwezi mmoja kutokana na maumivu ya nyama za paja.  

Mshambuliaji huyo wa kiholanzi alipata maumivu hayo wakati akipiga kopna katika mchezo wa ushindi dhidi ya Shakhtar Donetsk jumanne usiku na hatocheza tena mpaka mwakani.  

Kwa maana hiyo mshambuliaji atakosa mechi takribani 8 kwa mujibu wa kocha wake David Moyes.

Robin Van Persie atakuwa nje kwa mwezi mzima. Alipata maumivu  wakati akipiga kona katika dhidi ya Shakhtar. Ni wakati mbaya kwetu ukizingatia rekodi nzuri tuliyonayo pindi RVP anapocheza pamoja na Rooney na hawacheza pamoja kwa muda kiasi."

MECHI ATAKAZOKOSA ROBIN VAN PERSIE
Aston Villa (A), Dec 15, Premier League
Stoke (A), Dec 18, League Cup
West Ham (H), Dec 21, Premier League
Hull (A), Dec 26, Premier League
Norwich (A), Dec 28, Premier League
Tottenham (H), Jan 1, Premier League
Swansea (H), Jan 5, FA Cup
Swansea (H), Jan 11, Premier League



No comments:

Post a Comment