Search This Blog

Wednesday, December 11, 2013

HIGUAIN: SIKUWAHI KUZUNGUMZA NA KLABU YA ARSENAL KUHUSU KUNISAJILI


Kikosi cha Arsene Wenger kinacheza na Napoli usiku huu katika mechi ya kuamua msimamo wa mwisho wa kundi F katika michuano ya Champions League.

Na japokuwa Wenger alijaribu kumsajili  Higuain Arsenal, mshambuliaji huyu wa kiargentina anasisitiza hakuwahi kuzungumza na klabu hiyo ya kaskazini mwa London.

"Ndio," Higuain alijibu alipoulizwa na gazeti la  Times, kama kulikuwa na uwezekano wa kuhamia Arsenal katika kipindi cha kiangazi kilichopita.

"Lakini sikuwahi kuzungumza nao. Kulikuwa na mazungumzo baina ya Real Madrid na Arsenal, lakini ilikuwa ni Napoli ambao walikuja na kuninunua."

Wenger alidhani amefanikiwa kushinda vita ya saini ya Higuain kwa ada ya uhamisho kwa £23million lakini Napoli wakatoa ofa ya  £32m na kumsajili muargentina.

No comments:

Post a Comment