Search This Blog

Saturday, December 3, 2011

WENGER AKIRI YUPO TAYARI KUSAJILI - ASEMA CHAMAKH AONDOKI KWA MKOPO- KUMUACHA ALMUNIA JANUARY


Kocha Arsene Wenger amethibitisha kuwa yupo sokoni kutafuta wachezaji wazuri katika kipindi cha dirisha dogo la mwezi January.

Wenger anataka kuiboresha timu yake hasa katika safu ya ushambuliaji kwa kuwa na machaguo yaliyo bora tena kwa wingi wa kutosha, lakini amesisitiza hakuna nafasi ya mchezaji aliye nje ya form Maroune Chamakh kutolewa kwa mkopo japokuwa kumekuwa na interest kutoka kwa QPR na PSG.

“Kwa sasa, sifanyi chochote kuhusu usajili wa mwezi Janaury, nina kikosi kikubwa, lakini nikipata mchezaji mzuri na anayefaa katika mipango yangu then itabidi nimchukue.

“Kama tusipopata majeruhi, then tutakuwa hatuna shida kwa sababu tunae Chamberlain, ambaye anaweza kucheza pale, pia kuna kuna Park, Arshavin, na Van Persie. Hivyo bado tuna wachezaji wazuri wenye uwezo wa kumletea adui madhara, lakini tutapata shida sana ikiwa tutapata majeruhi.”

Wenger pia amesisitiza Chamakh-ambaye atakuwa na timu yake ya Morocco katika michuano ya kombe la mataifa ya Afrika mwezi January-anaweza kurudisha makali yake aliyoyaonyesha msimu uliopita alipowasili kutoka Ufaransa na hawezi kumruhus aondoke kwa mkopo in January.

“Ni vigumu kumtoa kwa mkopo sasa kwa sababu ya African Nations Cup in January, atarudi mwezi February hivyo atakuwa amechoka, so sio rahisi kumtoa kwa mkopo. Wachezaji watakaoenda Afrika wanahitaji wataondoka wiki mbili kabla ya michuano. Then watacheza ile michuano kwa almost 3 weeks, halafu wanahitaji kupumzika kwa wiki mbili jumla zinakuwa wiki 6.

“Chamakh sasa hivi ana tatizo la kutokujihamini na pia kukosa nafasi, lakini naamini atakapopata na nafasi na kuzitumia vizuri atarudisha makali yake.”- Wenger.

Wenger pia amekiri atamruhusu Manuel Almunia aondoke mwezi Janaury.

No comments:

Post a Comment