Search This Blog

Saturday, December 3, 2011

ANELKA NA ALEX WAONDOLEWA KIKOSI CHA KWANZA - WAPELEKWA KIKOSI CHA PILI NA AVB


Nicolas Anielka na Alex wamefungiwa kufanya mazoezi na kikosi cha kwanza cha klabu ya Chelsea na kocha Andre Villas-Boas.

Wachezaji hao wawili wote kwa sasa hawapo katika mipango ya mreno huyo na inaeleweka mbrazil Alex amepeleka ombi la uhamisho huku Anelka akiweka wazi anaondoka mwezi January na kuna uwezekano mkubwa akasajiliwa na big spenders wa kirusi Anzhi Machakhala.

Timu nzima ya Chelsea sasa ipo katika mshtuko kwa kitendo cha Villas-Boas, na wachezaji hao wawili kwa sasa wamekuwa wakifanya mazoezi na kikosi cha pili cha Chelsea huku wakivuta muda kuondoka Stamford Bridge.

No comments:

Post a Comment