Search This Blog

Saturday, December 3, 2011

MARTIN O'NEILL KOCHA MPYA SUNDERLAND


Klabu ya Sunderland imemtangaza rasmi kocha Martin O’Neill kuwa kocha wao mpya, akimbadili Steve Bruce.

Mtandao rasmi wa “Black cats” ulitangaza taarifa hiyo asubuhi ya leo, wakithibitisha kwamba O’Neill, 59, amesaini mkataba wa miaka 3 ya kuitumikia klabu hiyo.

O’Neill aliuambia mtandao huo: “Najisikia vizuri sana kuweza kurudi tena katika soka na kuwa manager wa Sunderland. Ni wakati mzuri kwangu mimi.

“Nimekuwa nikisikia uzuri wa klabu hii, lakini baada ya kufika hapa na kuuona uwanja na training ground, nimethibitisha uzuri wa klabu hii. Ni pazuri sana kiukweli.

“Natumai nitaisadia Sunderland kufanikiwa sana. Hilo ndilo lilonileta na ndio dhamira yangu.” Alisema O’Neill.

No comments:

Post a Comment