Search This Blog

Saturday, December 3, 2011

MASHABIKI WA YANGA WAISHANGILIA ZIMBABWE IKICHEZA DHIDI YA STARS

Mashabiki wa timu ya Yanga wakifanya kitendo ambacho si cha kizalendo kwa kuishangilia timu ya taifa ya Zimbabwe wakati wa mchezo wa kuwania kuingia robo fainali ya michuano ya TUSKER CECAFA CHALLENGE CUP 2011, uliofanyika kwenye uwanja wa Taifa jioni hii na Kilimanjaro Stars kufungwa goli 2-1 . Kitendo hicho kimelaaniwa na hata waandishi wa vyombo mbalimbali vya nje waliokuwa wakiripoti mchezo huo na kusema, "Hii haisaidii maendeleo ya soka na haijawahi kutokea katika nchi zao mashabiki wa nyumbani wakawashangilia wageni".

Akifadhaika zaidi mpiga picha wa Kenya Mohamed Amin, ametoa mfano kwamba wao kwa timu yao ya taifa wanaijali na kuipenda vilivyo, tofauti na vituko vya mashabiki wa Yanga alivyoviona leo. Anaongeza kwa kutoa mfano kuwa "Mwaka 1987 timu yao ya Harambee Stars iliwahi kuwa na wachezaji 12 wa timu ya Golmahia, na kati ya hao 12 wachezaji 9 walikuwa wakianza kipindi cha kwanza, lakini mashabiki hawakuwahi hata siku moja kufanya kitendo cha aibu kama hiki cha mashabiki wa Yanga" amemaliza Mohamed Amin, Mwana wa mpiga picha Maarufu wa ukanda huu wa Afrika Mashariki na kati mzee Mohamed Amin aliyepoteza maisha katika ajali ya ndege miaka kadhaa iliyopita.

Kilimanjaro Stars imefanikiwa kusonga mbele katika hatua ya robi fainali ambapo itashuka dimbani tarehe 6 mwezi huu kucheza na timu ya taifa ya Malawi.

1 comment:

  1. KWANZA LAZIMA TUKUBALI MAKOCHA HATUNA, SIASA ZA UZAWA NDIO HIYO LAANA INATUBEBA.TANZANIA KIPIMO CHA UKOCHA NI NINI? KUONGEA OVYO,MUDA AMBAO MTU KAJITANGAZA KUWA NI KOCHA, AU SENINA ZA WIKI KADHAA ZA UKOCHA NDIO TOSHA?.NACHOFAHAMU UKOCHA NI TAALUMA AMBAYO MTU ANABIDI AUDHURIE MASOMO HUSIKA KWA KIWANGO CHAKURIDHISHA NA SI MWALIMU WA CHEKECHEA UMPE SEKONDARI, HUU NI UZUSHI..NASUALA LA MASHABIKI WANAODAIWA KUWA NI WA YANGA KUSHANGILIA TIMU NGENI KIGEZO NI KIPI? WANASIFIKA MALAWI MASHABIKI WAO WANASHANGILIA MUDA WOTE BILA KUJALI TIMU YAO INACHEZA VIPI NA HAWANYAMAZI HATA KAMA TIMU YAO IMEFUNGWA JE HAPO MASHABIKI HAWA WAMESHANGILIA TIMU PINZANI? KWAKUWA HAWAKUNYAMAZA WAKATI TIMU YAO INAFUNGWA?
    TUACHE CHUKI ZA AJABU KWA KUOGOPA KUSEMA UKWELI KUWA KIWANGO CHA MAKOCHA KIDOGO. TIMU HAINA USHINDANI HADI TUPATE NAFASI ZA UPENDELEO?
    LAZIMA KELELE ZA UZAWA ZIISHE DUNIA MOJA HII WATU TUNATAKA MAFANIKIO NA SI KUENDEKEZA NJAA. WASIPO KUWA TAYARI KUKAA DARASANI NA KUSOMA HAKUNA JIPYA,WANATAMBA NA VYETI VYA MAUDHULIO YA SENINA NA SI VYA KUHITIMU TAALUMA YA UKOCHA.

    ReplyDelete