Search This Blog

Saturday, December 3, 2011

ANELKA NA ALEX NAO KUONDOKA CHELSEA JANUARY-AVB ATHIBITISHA



Game over: Anelka and Alex look to have played their last games for the BluesGame over: Anelka and Alex look to have played their last games for the Blues



Muda wa Nicolas Anelka na Alex @Stamford Bridge umeisha baada ya kocha Andre Villas-Boas kutangaza kuwa amekubali maombi ya wachezaji hao kutaka kuondoka Chelsea.

Wachezaji hawa wawili hawakuwa wamewekwa katika kikosi kilichosafiri kuelekea ST.James Park leo hii, na jana waliripotiwa kupigwa stop na AVB kushiriki katika mazoezi ya kikosi cha kwanza.

Chelsea wamethibitisha juu ya hatma ya Anelka na Alex mara tu baada ya timu hiyo kushinda mechi yake ya dhidi ya Newcastle.

Villas-Boas alisema: “Mazungumzo yangu na wachezaji(Anelka na Alex) yalikuwa fair and direct. Walionyesha nia ya kutaka kuondoka hapa, na wakaomba kupitia transfer request kwa muda sasa.

“NI wachezaji wa daraja la juu, ma-pro wa ukweli wasiona mashaka, lakini kwa muda huu na matokeo ya hivi karibuni, tumeamua ya kuyakubali maombi yao ya kutaka kuondoka ili kujaribu kupata wachezaji wengine watakaojaza nafasi zao kuweza kuimarisha kikosi chetu.”

No comments:

Post a Comment