Search This Blog

Friday, December 2, 2011

HARRY REDKNAPP NA SCOTT PARKER WANYAKUA TUZO ZA FA MWEZI NOVEMBA


Mwezi wa November umeonekana kuwa bora sana kwa Tottenham Hotspurs sio kwa matokeo uwanjani bali hata katika tuzo za mwezi huo kutoka kwa chama cha soka cha nchini England.

Kupitia tuzo za kila mwezi zitolewazo na FA, kocha wa Tottenham Harry Redknapp na kiungo Scott Parker wamefanikiwa kushinda tuzo wa kocha bora na mchezaji bora wa Barclays premier league kwa mwezi November.

Redknapp na Parker walikabidhiwa tuzo zao leo wakiwa mazoezini.

Mwezi uliopita wawili hawa kwa pamoja waliiongoza na kuiwezesha Spurs kushinda mechi dhidi ya Fulham, Aston Villa, and West Bromwich Albion.

No comments:

Post a Comment