Search This Blog

Saturday, December 3, 2011

WALIOMUITA STURRIDGE "NYANI" KUFUNGIWA MAISHA STAMFORD BRIDGE.


Klabu ya Chelsea imetishia kuwafungia maisha mshabiki au mashabiki wowote watakaokutwa na hatia ya kufanya vitendo vya kibaguzi dhidi ya wachezaji weusi ndani ya timu hiyo.

Hivi karibuni mchezaji mwenye asili ya kiafrika Daniel Sturridge alikutwa na mkasa wa kufanyiwa vitendo vya kibaguzi kutoka kwa mashabiki wa timu yake ya Chelsea.

Huku uchunguzi ukiwa unaendelea at Stamford Bridge baada ya malalamiko kutolewa na uongozi wa Chelsea kwamba baadhi ya mashabiki wenye uwezo wa kiuchumi walimuita ‘nyani’ Sturridge wakati wa mchezo wa Champions league dhidi ya klabu ya Genk, iliyofanyika nchini Ubelgiji wiki mbili zilizopita.

Hivyo klabu hiyo inafikiria kutoa adhabu ya kifungo cha maisha cha kutoingia uwanjani kwa watakaopatikana na hatia juu ya malalamiko hayo.

No comments:

Post a Comment