Search This Blog

Saturday, December 3, 2011

TEVEZ AENDELEA KUCHEZA GOFU KWAO, HUKU VILABU VYA ULAYA VIKIMGOMBEA.




AC Milan wanaamini wapo karibu kuweza kushinda vita ya kumsaini Carlos Tevez japokuwa wanapata upinzani mkubwa kutoka kwa mabillionea wapya kutoka Urusi Anzhi Makhachkala.

Man City wanataka mnunuzi amsaini Tevez kwa dili la kudumu mwezi January, huku Milan wameshatangaza kwamba watakuwa radhi kumsaini Tevez kwa mkopo huru huku wakipewa haki ya kumnunua mwishoni mwa msimu.

Ingawa, mtu wa ndani kutoka kwa mabingwa wa Serie A amesema kuwa City wapo tayari kupokea kiasi cha £2.6 ili kumuacha Tevez aende San Siro hadi mwishoni mwa msimu, according na gazeti la jiji la Milan maarufu kama Gazzetta dello Sport.

Tevez kwa sasa yupo zake Buenos Aires akipumzika na familia yake huku akicheza gofu katika viwanja mbalimbali akisubiri hatma yake na klabu yake ya Man City.

CARLOS TEVEZ AKIWA MKEWE KATIKA UWANJA WA GOFU JIJINI BUENOS AIRES-AREGENTINA.

Akiongea na Waandishi wa habari kocha wa Milan, Massimiliano Allegri ameutetea uamuzi wa kumtaka Tevez akisema: “Tevez ni mchezaji mkubwa, lakini ni mapema sana kumzungumzia.”

Kwa upande mwingine wa shilingi klabu ya Anzhi nayo imeingia katika vita ya kumnasa Carlitos, na wanaweza kwa urahisi kabisa kuilipa City zaidi ya £20m ili kumtia kibindoni Tevez ili ashirikiane na Samuel Eto’o. Timu nyingine ambayo imeonyesha nia kwa Tevez ni Dynamo Moscow, ingawa Milan wana imani na nafasi kubwa ya kumsaini Tevez kwa kuwa mchezaji pamoja na wakala wake wanaonekana kutokuwa tayari kuhamia Russia tena wakati huu baridi.

No comments:

Post a Comment