Search This Blog

Friday, December 2, 2011

HATMA YA ZANZIBAR CECAFA CUP


Safari ya Zanzibar Heroes katika michuano ya CECAFA Tusker Chalenji Cup itaamuliwa na sheria ya kumpata best losser, kufuatia goli la Amissi Cedric lililo wapa ushindi Burundi wa goli 1-0 pala walipowakabili Uganda.

Katika mchezo wa awali uliokuwa wa upande mmoja, Zanzibar Heroes waliichapa Somalia magoli 3-0, huku wakipoteza nafasi lukuki za kujipatia magoli zaidi.

Zanzibar Heroes iliyokuwa chini ya Kocha muingereza Stewart Hall, wakicheza bila ya mshambuliaji wao hatari Ally Badri Ally waliandika goli la kwanza kupitia kwa Selemani Kasim Selembe katika dakika ya 6 kufuatia makosa ya mabeki wa Somalia katika kuondosha mpira kwenye Hatari. Goli hilo lilidumu mpaka mapumziko.

Kipindi cha pili kiliendelea kwa Zanzibar Heroes kuutawala mchezo na ndani ya dakika 5 waliandika goli la pili kufuatia mpira uliomtoka kipa na kumkuta Abdul Halim Hamadi na kufunga goli la pili, huku la tatu likifungwa na beki Aggrey Morise. Mpaka filimbi ya mwisho Zanzibar 3-0 Somalia.


Katika mchezo wa pili ulishuhudia Waganda wakipoteza mchezo mbele ya Burundi kufuatia kwa goli la Amissi Cedric lililo dumu dakika zote za mchezo.

Katika mchezo huo ulio malizika kwa Burundi kuichapa goli moja Uganda. Waganda walipoteza nafasi kadha kupitia kwa washambuliaji wake walio ongozwa na Emmanuel Okwi.

Kwa matokeo hayo Burundi wanamaliza wakiongoza kundi huku Uganda wakiwa wapili. Zanzibar itabidi wangoje hekima za CECAFA kama watapata nafasi katika best loser.

No comments:

Post a Comment