Search This Blog

Thursday, September 20, 2012

KALI YA LEO: BARCELONA WAWAKATAA WAHUDUMU WA KIUME KWENYE NDEGE - WAOMBA WALETEWE MADEMU TU



Mwaka 2010, Turkish Airlines alilipa kiasi cha €7.7 ili kuwa wadhamini wa rasmi wa masuala ya usafiri, wakiwa wanahusika na kuwasafirisha ndani ya Spain na popote duniani.

Miaka miwili ndani ya mkataba huo, wakatalunya sasa wamepeleka ombi la kampuni hiyo ya kituruki kupeleka wahudumu wa kike tu kwenye ndege wanayopanda timu hiyo kwa ajili ya safari zao. Sababu kubwa waliyoitoa ni kwamba wahudumu wa kiume mara nyingi huwa wanasumbua kwa kuwa washabiki wao hivyo wanakosa utulivu safarini. Gazeti la kituruki Hurriyet linaripoti:

"Wahudumu wa kiumemara nyingin wanakuwa wanasumbua kwa kutaka autographs na jezi kutoka kwa wachezaji vipenzi vya mashabiki wengi duniani kama Lionel Messi na Andres Iniesta, jambo ambalo muda mwingine linakuwa kero kwa timu."

Kwa maana hiyo Turkish Airline wamekubali ombi la Barca na wamewachagua mademu 20 kwa ajili ya kuwahudumia Barcelona katika safari zao. Na hapo chini ndivyo Lionel Messi alivyopokewa taarifa hizo za watoto wa kike 20 kumuhudumia kwenye ndege.

No comments:

Post a Comment