Search This Blog

Thursday, September 20, 2012

''HAPA BAHANUZI,KULE KIIZA,NYUMA TWITE NA YONDANI,HATOKI MTU ' ZAIMALIZA YANGA.

Kocha wa Dar es salaam Young Africans Tom Saintfiet amesema kwamba kuanza vibaya kwa michezo yake ya ligi kuu kumetokana na baadhi ya wachezaji wake kujihisi wakubwa na muda mwingi wamekuwa wakitumia kubadilisha mitindo ya nywele na viatu. Akizungumza na Sports Extra mara baada ya mchezo kumalizika kwenye uwanja wa jamhuri jana kocha huyo amefafanua kwamba pia vyombo vya habari vimewafanya wajione wakubwa na hivyo muda mwingi wanatumia akili zao kufikiria namna ya kutokea katika vyombo habari badala ya kufikiria mchezo. Ama kwa upande mwingine kocha huyo amekiri kama amefungwa mchezo huo kihalali baada ya wachezaji wake kupata nafasi zaidi 8 na kushindwa kufunga bao ilihali mtibwa wamepata nafasi nne na kufanikiwa kupachika mabao 3. Aidha Tom ameongeza kwamba hakukuwa na tatizo la uwanja, mwamuzi wala Hoteli waliyofikia.

No comments:

Post a Comment