Search This Blog

Wednesday, September 19, 2012

SIMBA WAENDELEA KUTISHA LIGI KUU - WAWATAFUNA WANAJESHI WA JKT RUVU 2 - 0

Mabingwa wa Tanzania bara Simba SC leo hii wameendeleza makali yao waliyoanza nayo ligi kwa kuitandika timu ya wanajeshi wa JKT Ruvu kwa mabao mawili kwa sifuri.
Simba ambao walicheza mchezo kwa dakika nyingi baada ya mshambuliaji wao tegemeo Emmanuel Okwi kutolewa nje kwa kadi nyekundu kipindi cha kwanza cha mchezo, walipata mabao yao kutoka kwa kiungo Amri Kiemba aliyefunga bao la kwanza na Haruna Moshi Boban aliyepiga kidude cha pili.
Kufuatia matokeo hayo Simba inaendelea kukamata usukani mwa ligi kwa kukusanya pointi 6, magoli matano ya kufunga na wakiwa hawajuruhusu nyvu zao kuguswa. Simba walishinda mechi ya kwanza ya ligi kwa 3 - 0 dhidi ya African Lyon.
Kwa upande mwingine huko jijini Mwanza Azam FC wametoka sare ya kufungana 2-2 na Toto Africa, wakati Tanzania Prisons wametoka 1 - 1 na Coastal Union ya Tanga, Kagera Sugar wametoka sare tasa na JKT Oljoro, huku Ruvu Shooting wakiifunga Mgambo JKT 2-1.

 

No comments:

Post a Comment