Search This Blog

Wednesday, September 19, 2012

BAADA YA MIAKA 10 JUVENTUS WANARUDI KWENYE CHAMPIONS LEAGUE LEO - WAKIANDAMWA NA HISTORIA YENYE UTATA KATIKA MICHUANO YA ULAYA

 
Wakati fulani katika miaka ya 1980, wakurugenzi wa klabu ya Juventus walwakusanya kwa pamoja wachezaji wa kikosi cha kwanza cha klabu hiyo kuzungumza nao. Klabu ilikuwa na tatizo kubwa na ilibidi kulitafutia ufumbuzi: haikuwa imeshinda kombe la ulaya.

Kwa wakati huo, mshambuliaji Paolo Rossi alisema kitendo cha wao kutoshinda ubingwa wa ulaya ni 'ajabu'. Lakini hata baada ya Juventus walipofanikiwa kushinda ubingwa wa ulaya na kwa mara ya pili katika historia ya klabu hiyo mwaka 1996, klabu hiyo bado haijawa na mafanikio mazuri kwenye michuano hiyo.

Ni jambo la kushangaza kuona klabu yenye mafanikio kuliko zote nchini Italia ina rekodi isiyo nzuri kwenye michuano ya juu kabisa katika ngazi ya vilabu. Juventus wameshindana katika champions league mara 26 - idadi ya juu kuliko timu zote za ulaya kasoro AC Milan(26), Ajax na Bayern Munich (42), Dynamo Kiev (29), Benfica (31) na Real Madrid (42). Kati ya timu zote hizi ni Dynamo Kiev ndio ambayo imepata mafanikio kiduchu.

Kutokufanikiwa kwa Juventus kunaendelea mbele zaidi. Wamefanikiwa kufika katika nusu fainali ya klabu bingwa ya ulaya mara nyingi zaidi kuliko timu zote kasoro Manchester United, Milan, Barcelona, Bayern na Real lakini, kutokea hapo, timu hiyo iliyoshinda mara nyingi ubingwa wa Italia imeshindwa kuleta umwamba wake katika michuano ya UEFA. Juventus ni moja ya timu tatu, pamoja na Benfica na Bayern , zilizopoteza fainali za Champions league kuliko zilivyoshinda.

Na katika mechi zote hizo zilikuwa zikiandamwa na matukio yenye utata. Juventus walikuwa wakituhumiwa kutumia madawa ya kuongeza nguvu na upangaji wa matokeo huku balaa ya lilitokea katika mechi yao ya fainali dhidi ya Liverpool na kukatokea vifo vya mashabiki wengi -(Heysel Tragedy 1985)



Katika michuano yao ya kwanza ya ulaya msimu wa 1957-58 waliingia na aibu ya aina yake. Pamoja na kuwa wachezaji wawili waliokuwa bora kwa wakati huo Omar Sivoru na John Charles, walifungwa 7-0 na Wiener Sports Club na kutolewa kwenye mashindano.

Baada ya mchezo huo, Charles alilamika juu ya mchezo wa nguvu na rafu waliokuwa wakicheza Waustralia: "Mchezo huu ulikuwa wa kutisha zaidi tangu nianze kucheza soka. Nilipigwa mateke sana na niliumia kiasi madaktari walitaka kunifanyia upasuaji wa mguu ulioumia."

Juventus waliendelea kuusotea ushindi wao kwanza katika michuano hiyo. Baada ya kufungwa na CSKA Sofia msimu wa 1960-61, ikawabidi wasubiri mpaka jaribio lao la tatu, msimu uliofuatia, ambao Juventus wakashinda mechi ya ya kwanza, na wakawatoa Panathinaikos na Partizan Belgrade, na wakaenda kuwachafulia historia Real Madrid baada ya kuwafunga nyumbani kwao 1-0 katika dimba la Bernabeu - mchezo wa kwanza kwa Madrid kupoteza kwao. Katika mechi ya pili ya play off jijini Paris Madrid wakshinda 3-1.

Kutokufanikiwa kwa mabingwa wa Italia katika michuano ya Ulaya kulitoa picha ya matatizo ya ndani ya klabu ya ambayo ilikuwa inatawala vilivyo katika ligi ya ndani katika kipindi fulani, kama ilivyokuwa kwa Manchester United katika miaka ya mwanzo ya 90 na hata Real wenyewe mwishoni mwa miaka ya 70, kiwango cha waitaliano hakikuwa kikitosha kuweza kupambana katika michuano ya ulaya kwa wakati huo. Uwezo wao ulikuwa chini huku Real na Benfica wakiendelea na kuimarika vizuri.

Mpaka kufikia muda ambao Serie A imeimarika, hatua kubwa zilikuwa zimepigwa na miji mingine tofauti na Turin. Klabu mbili za jiji la Milan zikaimarika na wakawa na timu nzuri zilizoenda kutawala ulaya katika miaka  ya mwanzo ya 60 wakibeba makombe manne kati yao ndani ya kipindi cha miaka saba. Wakati huo pia Italia yote ikaanza kufuata mfano wa klabu za jiji la Milan.

Katika wakati wote wa miaka 60, Inter Milan walimuajiri mtu mmoja kutoka Hungary Deszo Solti. Kupitia utafiti wa mwandishi Brian Glanville wa gazeti la Sunday Times, ilifichuka siri kwamba Solti aliwahonga na pia alijaribu kuwahonga marefa wengi wa bara la ulaya . Refa mmoja aitwaye Gyorgy Vadas alimuambia Glanville namna alivyopewa fedha ambazo zingetosha kununua magari matano aina ya Mercedes ili kuhakikisha kwamba Real Madrid hawaendi mbele katika nusu fainali ya 1965-66.

Kwa wakati hu Solti alikua anafanya kazi Inter na secretary wa klabu hiyo Italo Allodi. Wakafukuzwa na unajua wapi walipata kazi mpya katika miaka ya mwanzo ya 70? Waliajiriwa kwenye klabu ya Juventus.

Refa mwingine akajitokeza, safari hii alikuwa mreno Francisco Marques Lobo, alimwambia mwandishi Glanville namna, kuelekea kwenye mchezo wa nusu fainali kati ya juventus na vijana wa Brian Clough Derby County msimu wa 1972-73, anasema Solti alimfuata akiwa na funguo yingi za magari mapya na kiasi cha fedha cha £5,00. Lobo akakataa kuchukua mlungula lakini vijana wa Clough wanasema kuna mtu mwingine alichukua rushwa baada ya kufungwa 3-1 katika mechi ya kwanza.

Kwa wakati huo. UEFA hawakuwa na kikosi cha uchunguzi wa matukio kama hayo. Juventus wenyewe hawakuwahi kuwashtaki Sunday Times kwa kuandika tuhuma zile lakini hawakushinda ubingwa wa ulaya.

Wakamuajiri kocha mpya, mtaalamu Giovanni Trapattoni, lakini pamoja na kuwa na rekodi nzuri, kocha huyo akiwa na Juventus alishindwa kuwa na matokeo chanya alipoingia kwenye michuano ya ulaya.

Trapattoni alikuwa na rekodi nzuri sana na Juventus katika michuano ya ndani lakini hali ilikuwa tofauti kila alipotia mguu kwenye UEFA. Katika majaribio matano, walitolewa nje katika kila hatua iliyopo ndani ya michuano hiyo, ikiwemo fainali ya 1983 waliyofungwa na Hamburg 1-0. Na baadae ikaja kutokea balaa la Heysel, ambapo watu 39 walipoteza maisha.

Baada ya kusubiri kwa muda kwa muda mrefu Juventus  wakafanikiwa kuwafunga Ajax mwaka1996 katika fainali ya UEFA Champions league na kufanikiwa kubeba ubingwa kwanza wa ulaya chini ya kocha wao mpya Marcello Lippi.

Katika msimu huo wa 1995/96, kocha wa Rangers Walter Smith alimwambia mwandishi wa habari Hugh Mcllvanney kwa mshangao. "Umeona mapaja ya yule Ravanelli?" alisema. "Unawaangalia wachezaji ambao wapo vizuri sana kwa upande wa misuli kuliko mchezaji yoyte tuliyenaye. Siku zote tumekuwa tikpata taabu ya kutafuta namna ya kushindana nao kimbinu na sasa wameongeza kitu kingine wana nguvu ajabu - vigumu kushindana nao." - alisema Walter Smith

Katika msimu wa 1982-83, Trapattoni ilibidi akanushe madai kwamba timu yake ilikuwa ikitumia madawa ya kutanua misuli. Katika miaka ya mwishoni ya miaka ya 90, klabu hiyo tena ilikumbwa na tuhuma hizo tena. Alikuwa kocha mropokaji Zdenak Zeman aliyepelekea kuanzishwa kwa uchunguzi wa kisheria na mwendesha mashtaka wa Turin Raffaele Guariniello,  ambaye alikuwa shabiki wa Juventus.

Uchunguzi ulipomalizika ikagundulika kwamba kuna madawa yalikuwa yakitumika visivyo, zikaondolewa dawa takribani 100 kutoka kwenye klabu hiyo, mwezi November 2004, jambo lilopelekewa kusimamishwa udaktarii na kufungwa jela kwa daktari wa klabu Riccardo Agricola. Miezi kadhaa baadae, mkuu wa taasisi ya kuzuia matumizi ya madawa michezoni, Dick Pound, akataka Juve wavuliwe makombe yote waliyoshinda katika miaka hiyo likiwemo kombe la ulaya mwaka 1996. Hilo halikuwezekana, baada ya Daktari Agricola alipokata rufaa na kushinda kesi na Juventus wakasafishwa juu ya tuhuma hizo. Ingawa mtoa tuhuma Zdenak Zeman aliendelea kushikilia msimamo wake juu ya utumiaji madawa wa Juve akisisitiza timu hiyo ilikuwa ikitumia vibaya madawa ya kifamasia. Tuhuma zake zilikuja kuacha pale Juventus walipkutwa na kesi nyingine ya upangaji wa matokeo  maarufu kama Skenddo ya Calciopoli.

Usiku wa leo Juventus wanarejea katika michuano ya mabingwa ulaya wakiwa kama mabingwa Italy kwa mara ya kwanza tangu msimu wa 2002-03, walipofungwa fainali na Milan, wanarudi wakiwa bila kocha wao mkuu Antonio Conte katika benchi. Kocha huyo, ambaye alicheza katika fainali ya mwaka 1996, amefungiwa kwa miezi 10 kwa kosa la kujihusisha na upangaji wa matokeo wakati akiwa katika klabu ya Siena. Jambo ambalo linaiweka historia ya klabu hiyo katika mashaka makubwa ya uadilifu.

No comments:

Post a Comment