Search This Blog

Friday, September 21, 2012

YANGA WAANZA KUTIMUANA - SENDEU, MWESIGA, KOCHA SAINTFIET ANUSURIKA APEWA ONYO KALI

Siku chache baada ya kuazna ligi kuu vibaya, uongozi wa klabu ya Yanga chini ya Mwenyekiti Yusuph Manji leo umeanza harakati za kujipanga upya kwa kufanya mabadiliko kadhaa kwenye safu ya uongozi wa klabu hiyo.
 
Katika kikao cha kamati ya utendaji wa klabu hiyo iliyokaa leo mchana chini ya makamu mwenyekiti Clement Sanga imefikia maamuzi ya kuwaondoa kwenye uongozi wa timu hiyo katibu mkuu wa klabu hiyo Celestine Mwesigwa, ofisa utawala Masoud Saad, na Luis Sendeu aliyekuwa msemaji wa klabu - sababu ikielezwa ni kushindwa kutimiza majukumu ipasavyo.
 
Katika hatua nyingine kamati ya utendaji imewabadilishia majukumu Philip Chifuka aliyekuwa mhasibu wa klabu, huku aliyekuwa meneja wa timu Hafidh Salehe nae akibadilishiwa majukumu. Meneja mpya wa timu atatangazwa baadae kidogo.
 
Nae kocha wa klabu hiyo Mbelgiji Tom Saintfiet aliepuka panga lilowakuta wenzie lakini amepewa onyo kali kwa kitendo chake kilichoitwa cha kuzungumza "ovyo" na uongozi wa klabu.
 

1 comment:

  1. kwa luis sendeu wala sishangai nilijua mda wowote atatimuliwa na hii walikuwa wanasubili sababu na wameipata coz jamaa hana analolijua kiukweli katika soka yani ni kichwa maji mara kadhaa nimekuwa nikielezea mahovyo hovyo yake ndani ya chumba hiki na leo limetimia yan lilikuwa kichwani hili kuwa jamaa hajui kitu ilaaaa magumashi tuu

    ReplyDelete